Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa Klabu hiyo ina malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho la ASFC na Kombe la Mapinduzi msimu huu wa mashindano wa 2021-2022 unaonza Septemba 27, 2021 kwa Ligi Kuu Bara.
Manara ameyasema hayo alipozungumza na Waandishi Habari jijini Dar es Salaam wakati wakijiandaa na mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kwenye dimba la Kaitaba mkoani Kagera siku ya Jumatano.
Amesema Wachezaji, Benchi la Ufundi, Viongozi na Wadhamini wa Klabu hiyo wamejipanga kuhakikisha timu hyo inafanya vizuri kutokana na kukosa mataji mengi katika misimu minne iliyopita jambo ambalo halina sifa nzuri kwa Klabu kama Yanga.
“Sherehe za kutwaa Ngao ya Jamii zimeisha tumesheherekea sana, sasa twendeni tukaanze msimu huu wa mashindano ili tulete mataji yote kwa Mabingwa wa Kihistoria, Yanga SC na hii ndio maana ya ‘Return of Champions’”, amesema Haji Manara.
“Kwenye mchezo wetu wa Ngao ya Jamii, Wachezaji wetu walicheza kwa viwango vya juu sana, hii yote ilichangiwa na kuchagizwa na mbinu bora za Benchi letu la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi wakiongozwa na Viongozi wa Klabu, Wadhamini Wetu”, ameeleza.
“Waangalie Aucho, kama mlimuona Boniface Mkwasa anacheza kama huyu Kiungo wa Uganda, tazama Bangala alivyocheza, Feitoto hata Kocha Amunike alisema huyu Kijana anafaa na anaweza kucheza Barcelona ya Hispania, na ukiangalia Amunike kacheza Barca!”.
Pia Manara amesema kuwa Wanachama, Mashabiki wa Klabu hiyo wanapaswa kuwa na umoja wakati msimu huu ukianza ili kufikia malengo hayo waliyoyaweka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...