NA YEREMIAS NGERANGERA..NAMTUMBO.
Wanafunzi wa kidato cha sita tahasusi ya HKL shule ya sekondari ya Pamoja wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wameibuka washindi wa ligi ya mbuzi iliyoshindanisha timu sita , tahasusi ya HGK kidato cha tano,tahasusi ya HKL kidato cha tano na HGL kidato cha tano.
Zingine ni tahasusi ya HGK Kidato cha sita,HKL Kidato cha sita na tahasusi ya HGL kidato cha sita ambapo katika ligi hiyo tahasusi ya HKL kidato cha tano na tahasusi ya HKL kidato cha sita waliingia katika fainali na tahasusi ya HKL kidato cha sita waliibuka washindi katika ligi hiyo kwa kuifunga tahasusi ya HKL kidato cha tano kwa magoli 3 kwa 1 na kujinyakulia mbuzi .
Mwalimu wa michezo wa shule ya sekondari Pamoja bwana Azizi Mtumbey alisema ligi hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila tahasusi kuonesha kuwa na timu bora ,uwezo wa kucheza lakini mwisho wa yote tahasusi ya HKL kidato cha tano na HKL kidato cha sita ndio waliofanikiwa kufika fainali na HKL kidato cha sita kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa magori 3 kwa 1.
Gori la kwanza la tahasusi ya HKL lilifungwa dakika 17 na mfungaji Fadhili makanga huku gori la pili lilifungwa na George Lugongo dakika ya 57 na dakika ya 78 tahasusi hiyo walipata gori la tatu kupitia mchezaji yuleyule aliyefunga gori la kwanza Fadhili Mkanga na gori moja la tahasusi ya HKL kidato cha tano lilifungwa dakika 49 na mchezaji Loi Nassari.
Mgeni rasmi katika mechi ya fainali hiyo alikuwa Solomon Hyera mwandishi wa vikao baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo pamoja na kuwapongeza tahasusi ya HKL kidato cha sita kwa ushindi aliwataka kuendeleza vipaji walivyonavyo ili kujiweka tayari katika ushindani wa soko la ajira lakin bila kusahau lengo lao la kupata elimu hapo shuleni.
Hyera aliwapongeza walimu wa shule ya sekondari ya Pamoja kwa kuwalea vijana hao kinidhamu na kuwaendeleza kitaaluma lakini akawaomba kipindi kijacho wawashindanishe wanafunzi wenye vipaji mbalimbali sio mpira wa miguu pekee.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...