MKUU wa Ofisi Ndogo ya Mpango wa Chakula Duniani(WFP) Neema Mina Sitta amesema kuwa wakulima 22,000 wa zao la Mtama, kutoka Wilaya za Kongwa, Bahi na Mpwapwa, wameuza tani 17,000 za zao hilo kwa msimu wa mwaka huu na kufanikiwa kujipatia Sh bilioni 9.
Amefafanua wakulima hao wamenufaika na kilimo hicho kupitia Program ya Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA), inayotekelezwa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kupitia Mpango Mkakati wa 2017 hadi 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari Sitta amesema kwa sasa wamefikia vijiji 203 kati ya zaidi ya 700 vilivyopo.
"WFP ni mpango ambao unafanya kazi kwa mtazamo wa kibinadamu kama kusaidia sekta ya kilimo, maendeleo, wakimbizi, afya na lishe ambapo kwa Dodoma umesaidia wakulima wa zao la Mtama kuongeza usalishaji".
Ameongeza WFP iliandika mradi wa kilimo himilivu katika wilaya za mkoa wa Dodoma na kupata ufadhili wa Sh. bilioni 1.7 kutoka Shirika la Maendeleo la Ireland (Irish Aid) ambapo matunda yameshaonekana kwa wakulima zaidi 22,000 kujpatia Sh. bilioni 9.
"Uamuzi wa WFP kuingia katika kilimo himilivu cha Mtama tumeweza kuunganisha wakulima na soko moja kwa moja na kuondoa madalali au watu wac katikati walikuwa wanachangia kushusha bei ya zao,"amesema.
Pia amesema kwa sasa bei ya zao la Mtama kilo moja inaunzwa hadi Sh 550 kutoka Sh 250 ya awali hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na kuhamsisha kilimo hicho.
"Tumekuwa tukitoa elimu kwa wakulima namna ya kulima kilimo bora na endelevu ambacho kitaweza kuingiza mapato yao na nchi,"ameeleza.
Sitta amesema kilimo cha Mtama ambacho kinalimwa katika mkoa wa Dodoma kinazingatia mfumo wa kilimo hai jambo ambalo linachangia kuwepo na uhakika wa soko kote duniani.
Amefafanua ushiriki wao kwenye kilimo ni kuhakikisha mkulima ananufaika na kilimo lakini pia ardhi inakuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.WFP kupitia ufadhili wa Irish Aid, wamefanikiwa kuongeza uzalishaji wa zao la Mtama.
Ameongeza kwa msimu huu wakulima wamezalisha zaidi ya tani 17,000 na kujipatia Sh bilioni 9 lakini hitaji ni kubwa zaidi hasa kutoka ndani na nchini Sudani Kusini,” alisema.Kwa msimu ujao wanatarajia uzalishaji kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa wilaya za Chemba, Kondoa, Dodoma na Chamwino.
Sitta amesema kwamba katika kutekeleza CSA wamekuwa wakishirikiana na Serikali kwa kutumia watalam wao wa kilimo hali ambayo inaleta ufanisi mzuri.
"Tumepokea ombi la Serikali katika kuanzisha program zakuongeza uzalishaji kwenye zao la alizeti ambapo matarajio yao ni kuingiza kwenye Mpango Mkakati wa WFP wa 2022 hadi 2027,"amesema.
Pia WFP imekuwa ikinunua mazao mengine kama mahindi kwa ajili ya kupeleka katika ofisi za WFP za nchi nyingine na kwenye kambi za wakimbizi za Nduta na Nyarugusu.
"Hadi sasa wamefanikiwa kununua zaidi ya tani laki saba kwa ajili ya kusambaza katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi,"amesema Sitta wakati akielezea hatua ambazo wanachukua katika kushirikiana na wakulima hao kulima zao la Mtama na kupata faida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...