Na Mwaandishi wetu wa Michuzi Tv
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema tamasha la utalii wa misitu linaloendelea Mkuranga katika hifadhi ya msitu wa mazingira asilia Pugu kazimzumbwi Safu ya Vikindu ni mwendelezo wa kuhamasisha utalii nchini kama alivyoanza Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha utalii kimataifa.
Akizungumza wakati akifungua tamasha la Utalii wa misitu katika msitu wa Vikindu Mkuranga mkoani Pwani na kuhudhuriwa na mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega na Wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Pwani Kunenge amesema wamedhamiria kuhamasisha utalii.
"Uongozi wa mkoa wa Pwani umedhamiria kuchochea na kuhamasisha utalii kwakutumia vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya mkoa wa Pwani. Katika wilaya za mkoa wetu kuna vivutio vingi vya utalii ambavyo wameanza kuhamasha ili kutumia vivutio hivyo kuburudisha pamoja na kuingiza kipato,"amesema.
Ameongeza mkoa wa Pwani pekee ndio una pwani yenye hifadhi yenye ufukweni wa bahari ambayo mtalii akienda anaona wanyama na akihitaji kuogelea anaogelea sambamba na kuendelea kuangalia vivutio vilivyopo baharini hapo hapo.
"Kule kwenye hifadhi ya Saadani katika wilaya ya Bagamoyo kuna hifadhi ya taifa ambayo ukienda utafurahia kuona wanyama hifadhini sambamba na kufurahia Utalii wa uliopo baharini," amesema Kunenge.
Akizungumzia vivutio vilivyopo katika wilaya ya Mafia Kunenge amesema Wilaya hiyo pia ina vivutio vingi vizuri ambavyo havipo sehemu nyingine nchini hata duniani kote.
"Wilaya ya Mafia kuna vivutio vya utalii wa aina mbalimbali pamoja na kucheza na samaki aina ya Papa potwue ambaye ni kivutio kikubwa nchini," amesema Kunenge.
Pia amesema kukamilika kwa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere nao itakuja kivutio kingine kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi na kutuongezea mkoa na taifa kipato.Tamasha hilo la kuhamasisha utalii wa misitu nchini lilifunguliwa rasmi na Oktoba 1,2021.
Kwa upande wake Mbunge Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi misitu nchini.
Amesema vyanzo vingi vya maji yanayotumika kwa shughuli za majumbani, mashambani, viwandani na kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ni misitu.
Mchango wa utalii utaongezeka kama tutahamasisha na kuimarisha utalii ikolojia na kuhamasisha utalii wa ndani," amesema na kuongeza anafahamu wizara ilikasimu usimamizi wa vituo sita vya malikale kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania .
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakhar Kunenge akizungumza na washiriki wa mbio za Tamasha la Utalii wa Misitu katika msitu wa Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, akizungumza na washiriki wa mbio za Tamasha la Utalii wa Misitu katika msitu wa Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.ambapo amewaomba Watanzania kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuiweka miili yao vizuri na kujenga hamasa ya kufanya kazi.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Caroline Malundo, akizungumza na Michuzi Tv baada ya kushiriki mbio za Tamasha la Utalii wa msitu wa Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ambapo amewaomba wananchi wilaya hiyo kulinda na kuhifadhi wa misitu kwa ajili ya kizazi cha Mchango wa utalii utaongezeka, tutahamasisha na kuimarisha utalii na kutunza ikolojia na kuhamasisha utalii wa ndani hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakhar Kunenge akimvalisha medali ya washindi wa mbio za Tamasha la Utalii wa msitu wa Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. kushoto Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega.
Msanii wa muziki Bongo Fleva, Aslay akifanya yake kwenye Tamasha la Utalii wa msitu wa Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Abubakhar Kunenge kushoto akiwaanga wananchi waliojitoka baada ya Tamasha la Utalii wa msitu wa Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.kulia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...