Na Mwandishi Wetu, Pwani

MAMLAKA  ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),imeteketeza hekari moja ya shamba lenye mimea ya bangi katika kitongoji cha Kimereme, kijiji cha Nyani, Kata ya Mafisi, wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

Sambamba na uteketezaji huo, Mamlaka imewakamata watu wawili ambao ni wamiliki wa shamba hilo.Watu waliokamatwa ni Khamis Mohamed Tengeneza (59) kabila mzaramo na Abdallah Mohamed Hemba (48) kabila mzaramo wote wakazi wa Kiremeta.

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2,2021 kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Mamlaka hiyo Florence Khambi amesema shamba hilo limetekezwa Oktoba 1 mwaka huu sambamba na kukamatwa watu hao.

"Watuhumiwa wametenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 11(1) (a) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015 kama ilivyorejewa mwaka 2019,"amesema.

Amefafanua mpaka sasa watuhumiwa wameshikiliwa na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika.

 


 
Khamis Mohamed Tengeneza (59)


Abdallah Mohamed Hemba (48) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...