Naibu Katibu wa Habari ,Uenezi na Mahusiano na Umma  wa ACT Wazalendo Janeth Rithe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mikakati ya Chama na taarifa mkutano wa Halmashauri Kuu ulioketi hivi karibuni.




*Ni katika uchaguzi wa mwakani na kujiimarisha kuchukua dola 2025

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

CHAMA cha ACT Wazalendo kimetangaza kupitia mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika hivi karibuni kimetangaza kufanya uchaguzi zilizoachwa wazi kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao ikiwemo na Kifo cha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika  Januari 29 ,2022 ikiwa ni kuimarisha chama kwa kuwa na safu nzima wa viongozi kitaifa pamoja na mikakati ya chama kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Hayo aliyasema Naibu Katibu wa Habari ,Uenezi na Mahusiano na Umma wa Chama hicho Janeth Rithe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika kuelekea uchaguzi huo,amesema Chama kimezidi kujiimarisha ikiwa ni kuwajenga wanachama kiitikadi ya kuchukua Dola katika uchaguzi wa 2025.

Rithe amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar Juma Duni Haji ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na nia yake ya kugombea Uenyekiti wa Chama hicho ili nafasi mbili kuwa wazi na kugombea wanachama mwingine.

Amesema Halmashari kuu imeridhishwa na ngome ya vijana inavyofanya kazi katika kuwasemea vijana ikiwa ni pamoja na kumteua Sevelina Joseph Mola kuwa na Naibu Katibu Bara wa Ngome ya Vijana Taifa.

Aidha amesema kuwa ngome ya Wanawake imevunjwa kwa sababu ya kutofanya vizuri kwa upande wanawake na kuundwa kwa kikosi kazi cha kufanya ngome hiyo isimame kutetea wanawake kwa kuweka umoja wenye nguvu.

Amesema kikosi kazi cha kuimarisha ngome ya wanawake kitaongozwa Mwenyekiti Pavu Abdallah Juma ,Katibu Bonifasia Mapunda na wajumbe watatu ambao ni Halima Ibrahim Mohammed, Annamarrystella Mallack, pamoja Sevelina Mwijage.

Aidha Chama kimesema kitaendelea kupigania maslahi ya wananchi pamoja na machinga kwa mwenendo unaonekana una dosari.

ACT Wazalendo kimemteua Profesa Omar Fakih Hamad wa Jimbo la Pandani na Mnadhimu kwenye Baraza la Wawakilishi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...