*Ni Mtu mwenye Ualbino na kuomba vyombo dola kufanya uchunguzi dhidi ya waliofanya hivyo.
*Yadai kuwa kuamini uchawi kwa karne hii imepitwa na wakati
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
KITUO cha Sheria na Haki za Binadami (LHRC) kimesikitishwa na kulaani kitendo cha tukio la kufukuliwa kwa kaburi la Marehemu Heri Shekigenda Kijangwa aliekuwa na ualibino na kunyofolewa mguu.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga amesema marehemu huyo alifariki Julai 4 mwaka 2020 kwa maradhi ya kansa ya ngozi akiwa na umri wa miaka 45 na mwili wake kuhifadhiwa kwenye nyumba ya milele Julai 7 /2020 katika kijiji cha Tanda wilayani Lushoto mkoani Tanga.
“Katika hali isiyo ya kawaida baada yakupokea taarifa ya kufukuliwa kwa kaburi la Marehemu, Heri Shekigenda Kijangwa mnamo tarehe 24 Oktoba 2021 kufanywa na watuwasiojulikana kilisikitisha dhidi ya watu hao walinyofoa mguu wake wa kulia na kutoweka nao kusikojulikana" Amesema Henga.
Aidha kwa mwaka 2021 tukio hilo ni la pili kuripotiwa ambapo mei 3 na 4 mwaka huu iliripotiwa kwamba mwili wa mtoto mwenye ualbino aliyekuwa na umri takribani miaka mitano uliokotwa ukiwa umekatwa mikono yote miwili huko kijiji cha Nondo Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora ambapo hadi leo taarifa ya uchunguzi haijatolewa na Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Chama cha watu wenye ualibino Tanzania (TAS) Mussa Kabimba amesema kuwa kitendo cha kufukua mwili wa marehenu Heri Shekigenda Kijangwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 127 na 128 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.
Hatahivyo ameihimiza serikali na Jeshi la Polisi kuhakikisha kwamba kesi hiyo haitaishia kwenye ngazi ya upelelezi badala yake watuhumiwa wote wafikishwe mahakama na adhabu kali itolewe ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Amesema kuwa jamii inatakiwa kubadilika kwa karne hii sio ya kuamini uchawi ambao hauna nafasi ya kuweza kujipatia kipato bali wanatakiwa kufanya kazi kwa ubunifu kwa kutumia wataalam katika kada mbalimbali za taaluma.
Henga amesema suala utu ni muhimu sana kwani kufukuliwa kwa kaburi na kunyofoa baadhi ya viungo haikubaliki na kutakiwa kukemewa kila mmoja wetu katika ustawi wa taifa na duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...