Na Mwamvua Mwinyi,KIBAHA
DARAJA la Lumumba linalounganisha wilaya ya Kibaha na Ubungo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kuwa limetumia gharama kubwa lakini halitumiki .
Kufuatia malalamiko hayo ,Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Sara Msafiri alitembelea daraja hilo wakati wa ziara yake ya kikazi kata ya Pangani lililopo daraja hilo na kata ya Mkuza ,ambapo aliiagiza wakala wa barabara mjini na Vijijini not(TARURA)na, uongozi wa kata wafanye tathmini ya kina ya ujenzi huo .
Aliwataka ,kuainisha kazi zilizofanywa na kumpatia ripoti sahihi ofisini kwake ili kukiridhisha na gharama zilizotumika .
Sara pia aliwashukuru wananchi, kwa kuchangia ujenzi wa daraja milioni 60 hivyo kuwaomba viongozi husika kutoa mrejesho wa mara kwa mara kwa jamii kuhusiana na matumizi ya fedha zao .
Awali diwani wa kata ya Pangani,Augustino Mdachi alieleza,baada ya kero hiyo iliyodumu muda mrefu ,mwaka 2016 aliomba Jeshi la Wananchi Tanzania kuwapatia daraja la muda ambapo walipatiwa lililokuwa Mpwapwa ambalo lina uwezo kupitisha uzito usiozidi tani 10.
"Lilisafirishwa kwa msaada wa kampuni ya madalali wa Bima Tanzania kwa kuchangiwa mafuta ya sh.milioni 15.
Mdachi alifafanua TARURA ilihusika katika msaada wa kulifunga na wananchi walichangia chakula cha mafundi eneo la kazi pamoja na vifaa vingine vilivyogharimu milioni 60.
Kaimu Meneja TARURA Kibaha,Donald Mjale alisema, katika kukamilisha daraja Serikali kupitia TARURA imeshatumia milioni 80 kwa ajili ya ununuzi wa kokoto tani 60,waya,bolt na kuchimba mtaro wa kuchepusha njia ya maji ili kupunguza hatari ya kuharibu kingo za daraja.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha,Mshamu Munde aliitaka TARURA kuweka wataalamu na wabunifu kwenye daraja hilo kwani utaalamu wao bado unahitajika ili kuwa na daraja bora
Alimuomba diwani wa kata kufanya ufuatiliaji Jeshini ili kupata taarifa kamili Kama daraja walilopatiwa ni la muda ,au wameazimishwa ili Kama Ni la muda ufanyike utaratibu wa kujenga daraja la kudumu siku zijazo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...