Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa AKO Group akizungumza kuhusiana na kampuni hiyo kuipatia photocoy machine Shule ya Sekondari Urafiki.
Makabidhiano ya mashini ya Kudurufu Karatasi 'Photocopy machine'kati ya wanafunzi na mwalimu wa shule ya Sekondari Urafiki pamoja na uongozi wa AKO Group Limited katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa AKO Group Limited Selina Koka akitoa maelezo juu msukumo ulioifanya Shule ya Sekondari Urafiki kupata msaada wa mashine ya kisasa ya kudurufu karatasi.
Picha mbalimbali mara baada ya kufanya makabidhiano ya Photocopy Machine katika shule ya Sekondari Urafiki jijini Dar es Salaam.
*Ni kwa kutoa mashine ya kisasa kudurufu karatasi.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KAMPUNI ya AKO Group Limited imetoa msaada wa mashine ya Kisasa ya kudurufu karatasi )Photocopy Mashine ) katika shule ya Sekondari Urafiki ili kurahisisha baadhi ya shughuli katika shule hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hiyo Mkurugenzi wa AKO Group Selina Koka amesema kuwa msaada ulitokana na maombi ya shule hiyo katika mahafali ya kidato cha Nne yaliyofanyika hivi karibuni akiwa Mgeni rasmi wa mahafali hayo.
Koka amesema kuwa msaada huo ni kurudisha kwa jamii kwa kile kinachopatikana na kuona shule ya urafiki inauhitaji wa mshine hiyo na kuachana kutoa fedha kwenda kupata huduma za kudurufu karatasi nje ya shule.
Amesema licha ya kutoa mashine hiyo wanawajibu wa kushirikiana na shule pale wanapokuwa na uhitaji kutokana na ukaribu wa shule hiyo kwa Kampuni ya AKO Group.
Koka amesema kuwa msaada huo kutaongeza ari kwa walimu kuendesha mitihani mara kwa mara na hatimaye kuwa na ufaulu wenye tija katika matokeo ya kidato cha Nne Kitaifa
"Tumedhamiria kwenda kuwaunga mkono shule ya Sekondari Urafiki kwa mategemeo ya kufanya vizuri kwani wanafunzi wakitoka vyuoni wanaweza kuja kufanya katika kampuni ya AKO kutokana na mbegu tuliyoipanda"amesema Selina Koka.
Nae Mkurugenzi wa Rasilimali wa Watu AKO Group Daniel Chumu amesema kuwa ni uhakika wao mashine hiyo wataitunza ili waendelee kufaidi.
Amesema kuwa kazi ya wanafunzi ni kusoma kwa bidii ili kuleta matokeo chanya ya mashine hiyo kwenye uandaji wa mitihani ya ndani ya shule.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Wenceslaus Mutyama amesema kuwa AKO Group Limited wameona mbali kwani walikuwa na uhitaji wa mashine hiyo kwa muda mrefu.
Amesema kuwa watu wengine waigi mfano wa AKO katika kuwasaidia shule katika maeneo mbalimbali kwa wanafunzi wakifanya vizuri ni faida kwa taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...