Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKURUGENZI wa Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ,ameanza kupitia maeneo ambayo vyumba vya Madarasa vinajengwa kwa fedha aliyotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ikiwa ni Mkopo kutoa IMF ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na UVIKO-19.

Akiwa shule ya sekondari Simbani,Mhandisi Munde pamoja na mambo mengine hajaridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kwamba ametoa maelekezo ya jumla kuhakikisha kila shule inakamilisha kwa wakati.

Aidha,ameshangazwa kuona kamati za manunuzi hazijafanya mchakato wa madawati ilihali fedha ilitolewa siku moja na kwamba kitendo hicho ni kiashiria cha kuchelewesha mradi.

Mhandisi Munde ametoa rai kwa wajenzi na wasimamizi kuhakikisha kazi inafanyika usiku na Mchana ili ifikapo tarehe 5 Disemba,2021 Madarasa yote yawe yamekamilika tena kwa viwango na ubora unaotakiwa.

Halmashauri ya Mji Kibaha imepata kiasi cha Tsh.940,000,000.00 zinazojenga vyumba vya Madarasa 47 pamoja na Madawati ili kukabiliana na ongezeko kubwa la Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza Januari,2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...