Na Khadija Seif, Michuzi TV
MAONYESHO ya Jukwaa la “Swahili Fashion Week” Kwa zaidi ya Miaka 14 yanatarajiwa kufanyika Desemba 3, 4 & 5, mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi Wahabari Muasisi wa jukwaa la “Swahili Fashion " Mustafa Hassanali amesema ana matumaini ya kuimarisha msingi wa ubora wa jukwaa hilo na kwa shauku kubwa anasema Lengo la kuendeleza tasnia ya ubunifu Afrika bado linabaki kuwa kipaumbele, kupitia jukwaa hili na mtandao wake mkubwa wa vyombo vya habari, watumiaji wa bidhaa za ubunifu wa Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla sasa wataona mbadala wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje.
Mustafa amesema zaidi ya wabunifu sitini (60) wataonyesha vipaji vyao katika jukwaa hilo jijini Dar es Salaam Huku akisisitiza jukwaa hilo Swahili inaungana na serikali kusherehekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
"Jukwaa kubwa la Maonyesho ya mavazi Afrika la jukwaa la ‘Swahili Fashion Week' limepanga kufanya Maonyesho yake Desemba 3, 4 na 5 mwaka huu, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Maonyesho haya ya kumi na nne ya “Swahili Fashion Week" yataendelea kuwa kioo kwa maonyesho mengine ya mavazi Afrika kwa wabunifu wa Kitanzania, ukanda wa Afrika Mashariki hata wale wa kimataifa kwa mvuto na mandhari yake ya kipekee inayoendana na kauli mbiu ya jukwaa ya Tambua Kinachoipendezesha.
Jukwaa la "Swahili Fashion Week" inashirikiana na Serikali na wananchi kusherekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara ikiwa na dhamira ya kuonyesha ubunifu wa kupendeza, ubora na uzuri wa nchi, ili kuitangaza na kuongeza uchumi.
Jukwaa pia linawahimiza wabunifu wachanga kutumia jukwaa hili, ikiwa ni hatua moja wapo katika kukuza vipaji vyao vya ubunifu kwa mara nyingine kutakua na shindano la wabunifu chipukizi linalojulikana kama “Washington Benbella Emerging Designers Competition” ambapo wabunifu 10 wanatarajiwa kuonyesha umahiri wao kwenye ubunifu kupitia jukwaa hili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...