Na WAMJW - DOM. 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo ameelekeza Wizara yake kila idara  kuwa na dawati maalum la kuratibu tathmini ya kazi kwa 'score card' ili kupima viashiria vya ubora wa huduma wanazopata wananchi kutokana na mipango iliyowekwa. 

Dtk. Gwajima ameyasema hayo leo alipokutana na kikosi kazi cha Wizara ya Afya na Wadau wake ambacho kinahusika na kuandaa utaratibu mzima wa kufanya uhakiki wa ubora wa huduma za kitabibu na Uuguzi  zinazotolewa kwa wagonjwa (Clinical Service Performance Auditing). 

"Naelekeza Sasa kila idara iwe na dawati la uratibu wa tathmini ya viashiria vya ubora wa huduma wanazopata wateja kulingana na mipango iliyowekwa, juhudi za wadau wote zielekezwe eneo hili ngazi zote Ili tupongezane kwa takwimu  za viashiria 'clinical performance score cards." Amesema Dkt. gwajima. 

Amesema, ukiacha medicine performance auditing na hii clinical performance auditing, Wizara inaandaa pia customer service performance auditing inayoongozwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, lengo likiwa  kuihamisha Sekta ya afya kwenda kwenye performance auditing zenye score cards. 

Akieleza faida za uhakiki ubora wa huduma za afya Dkt. Gwajima amesema, inasaidia kuchochea motisha kwa watumishi, kufikia ubora wa huduma, mteja kuridhika, kuchochea medical tourism, uthibitisho wa vituo na kuleta tija kwenye Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na kupunguza malalamiko kwa wateja. 

"Faida za uhakiki wa ubora wa huduma za afya ni pamoja na kuchochea motisha kwa watumishi, kufikia ubora wa huduma, mteja kuridhika, kuchochea medical tourism, accreditation ya vituo pia tija kwenye Sheria ya Bima ya Afya kwa wote. Hivyo kupunguza malalamiko kwa wateja."Amesema. 

Aidha, Dkt. Gwajima amesisitiza ushirikishwaji wa karibu wa Idara zote  na Wadau wengine ndani na nje ya Sekta  ili kuchochea kasi katika maendeleo ya Sekta ya Afya. 

Pia kuwe na mwongozo utakaoelekeza utendaji wa pamoja wa wadau wote, hii itasaidia kuchukua hatua shirikishi kupitia viashiria vya score card ngazi zote. Alisisitiza Dkt. Gwajima. 

Hata hivyo, amewashukuru na kuwapongeza kikosi kazi cha Wizara ya Afya na Wadau wake ambacho kinahusika na kuandaa utaratibu mzima wa kufanya uhakiki wa ubora wa huduma za kitabibu na uuguzi na kuifikisha ndoto ya siku nyingi ya kuwa na "clinical services performance audit" ili kutimiza uhakiki wa ubora wa huduma kwa mteja. 

Nae, Mkurugenzi Msaidizi anaesimamia Hospitali za Rufaa za Mikoa Wizara ya Afya Dkt. Caroline Mayengu amemshukuru Waziri wa Afya kwa maelekezo na ushauri aliotoa ili kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa na kuahidi kutomwangusha katika kuboresha Sekta ya Afya nchini.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...