Rais Msaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza mara baada ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
JAJI wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, Jaji Imani Aboud amezishauri Mahakama Barani Afrika kufanyia kazi changamoto zinazozikabili Mahakama ikiwemo utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa.
Ameyasema hayo leo Novemba 3,2021 mara baada ya kuhitimisha matembezi ya kuadhimisha miaka 15 ya mahakama hiyo tangu kuanzishwa kwake, yaliyoanzia katika viwanja vya Leanders Kinondoni hadi Police Oficers Mess Osyerbaay jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa wakati sasa mahakama ianatimiza miaka 15 wameshafanya mikutano mikubwa ya Kimataifa miwili ambapo pamoja na mambo mengine wamekuwa wakijadili zaidi changamoto zinazojitokeza katika kutekeleza maamuzi yanayotolewa na mahakama hiyo ili waweze kujua ni namna gani wanaweza kuatua changamoto hiyo na kuweza kupata Suluhu kwani utekelezaji wa maamuzi ya mahakama hiyo umekuwa ni changamoto kubwa.
Jaii Imani amesema kuwa tangu Mahakama hiyo imeanza kazi imepokea kesi 300 ambapo imeweza kusikiliza kesi zaidi ya 150 huku maamuzi asilimia 17 hadi 18 yalitotolewa yametekelezwa kwa kiasi na asilimia zaidi ya 75 hayajatekelezwa kabisa.
"Maamuzi tunayoyatoa tunaamini kabisa ni maamuzi ya haki dhidi ya kama ni nchi, tunasema dhidi ya nchi kwa sababu mashauri mengi yanaletwa kulalamika kwamba nchi husika imevunja haki za binadamu ama kwa mtu mmoja au kikundi cha watu na katika utoaji haki lazima uhakikishe maamuzi yako au uone maamuzi yako yanatekelezwa, Lakini changamoto kubwa imekuwa maamuzi ya mahakama hayatekelezwi na nchi husika, mpaka sasa ni asilimia saba tu ya maamuzi yote tuliyotoa ndio yameweza kutekelezwa kabisa na asilimia 17 hadi 18 yametekelezwa kwa kiasi huku asilimia zaidi ya 75 ikiwa haijatekelezwa kabisa". Amesema Jaji Imani.
Amesema changamoto ya kutotekelezwa kwa maamuzi ni kubwa katika Mahakama kwani kazi ya mahakama hiyo ni kutaka kusikiliza mashauri na kutoa hukumu na kuona zinatekelezwa ili yule ambaye amekuja kudai haki amepata haki yake.
Ameongeza kuwa, hata hivyo mahakama iko kwenye mkakati wa kutafuta namna ya kumaliza changamoto hiyo ili waweze kupata ufumbuzi kupitia kikao cha siku tatu ambapo Mataifa mbali mbali ya Afrika yaliyoanzisha mahakama hiyo wanazungumza.
"Tumekuwa na mazungumzo na waliyoianzisha mahakama hii ambao ni Mataifa mbali mbali ya Afrika. Mataifa yote 55 tuzungumze kwa nini maamuzi yanayotolewa na mahakama hii hayatekelezwi, changamoto gani, na kama zipo ni namna gani tunatafuta suluhu ya kuziondoa sababu wanavyokuwa hawatekelezi sisi hatujui lakini kwa mikutano hii tumekuwa tukizungumza na nashukuru wawakilishi wa nchi mbali mbali wamekuwa wazi pamoja na wadau mbali mbali hivyo leo wakati tunafunga mkutano wetu wa siku tatu tutapata majibu ya namna bora ya kutafuta Suluhu ya kutatua changamoto". Amesema Jaji Imani
Kwa upande wake, Rais Mstaafu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza jaji wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu, Jaji Imani Aboud kwa kuamua kufanya matembezi ya kusheherekea miaka 15 ya mahakama hiyo.
Kikwete amewapongeza kwa hatua waliyoifikia kwa kufanya kazi vizuri na kazi kubwa kwani ilianzishwa Kipindi Dkt. kikwete alipokuwa waziri wa mambo ya Nje.
Amesema kuwa walisaini itifaki ya mkataba wa kuanzisha Mahakama ya hiyo hapa nchini pia wakaomba Tanzania kuwa mwenyekiti wa mahakama ya Afrika.
"Ninashukuru sasa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu kwa kukaa miaka 15 hapa nchini na sasa wamekuja Dar es Salaam kuja kufanya kumbukumbu ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwake
Rais wa Makahama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
Rais Msaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, mara baada ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
Rais Msaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay mara baada ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
Rais wa Makahama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu akizungumza mara baada ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
Rais Msaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay mara baada ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
Rais Msaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wengine wa mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo katika viwanja vya Polisi Oficers Mess kwaajili ya Kuhitimisha Matembezi ya kuandhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders na hukitimishwa katika ukumbi wa Polisi Oficers mess Masaki leo Novemba 3, 2021.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay wakionesha mabango wakati wa kuadhimisha miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu leo Oktoba 3,2021 jijini Dar es Salaam.
Matembezi ya maadhimisho ya miaka 15 ya mahakama ya Afrika ya haki za bianadamu na watu yaliyofanyika leo kutokea viwanja vya Leaders hadi Polisi Oficers Mess Masaki jijini Dar es Salaam.
Bendi ya polisi iliyoongoza matembezi ya Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu wakiongoza maandamano hayo yaliyoanzia katika viwanja vya Leanders na kuhitimishwa katika eneo la Ukumbi wa Poalisi Oficers Mess Masaki jijini Dar es Salaam leo Oktoba 3, 2021.
Viongozi mbalimbali wa kutoka nchi wanachama wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu wakiwa na bendera za nchi zao kabla ya kuanza Matembezi ya kuadhimisha Miaka 15 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...