Na Pamela Mollel,Arusha
Jamii imetakiwa kuyapokea matokeo ya utafiti wa wataalamu ili ipate majibu ya vikwazo changamoto wanazokutana nazo katika maisha yao.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa bodi ya chuo Cha uhasibu Arusha Dr Mwamini Tulli wakati akizungumza katika kongamano la pili la uvumbuzi na ubunifu lililofanyoka katika chuo hicho.
Amesema kuwa kufuatia tafiti zinazofanywa na wataalamu jamii inapaswa kupokea majibu yake na kuyakubali matokeo ili wapate majibu ya vikwazo wanavyokutana navyo katika maisha yao ili wasiwe wasindikizaji katika Safari ya maendeleo.
Aidha amewataka vijana wanaoshiriki kongamano Hilo kutumia matokeo ya tafiti hizo kwa manufaa ya jamii na taifa badala ya kubaki kuwa Mali yao.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho profesa Eliamani Sedoyeke alisema kuwa kupitia kongamano Hilo wataalamu watafanya mijadala ya kinifu katika tafiti ,bunifu na vumbuzi na kuja na mapendekezo ya kuendeleza teknolojia zinazozalishwa nchini.
Sedoyeke akifafanua kuwa matarajio yao Ni kuyafanyia kazi mapendekezo na kila watakachokijadili ili waweze kufikia malengo ya kutumia suluhishi bunifu katika kutatua matatizo ya jamii na taifa.
Mwenyekiti wa bodi ya chuo Cha uhasibu Arusha Dr Mwamini Tulli (aliyevalia kitenge) wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa chuo Cha uhasibu na wataalamu wa tafiti Mara baada ya ufunguzi wa kongamano la pili la ubunifu na uvumbuzi Lili lofanyika chuoni hapo
Mmoja wa kijana aliyeshiriki kongamano hilo akionyesha ubunifu wa picha kwa mgeni rasmi






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...