Na Amiri Kilagalila, Njombe
WAUMINI wa kanila la Makambako Christian Center MCC wamelazimika kuahirisha ratiba zote za ibada na kufanya maandamano huku wakishinikiza kurejeshwa kwa mchungaji wao wanaedai kuondolewa kanisani hapo na mwenyekiti wa Ushirika wa makanisa Tanzania TFC.

Waumini hao wamelazimika kuandamana wakimshinikiza mwenyekiti wa Tanzania fellowship church kumrejesha aliyekuwa mchungaji wa kanisa hilo kwa kile walichokieleza kwamba ameondolewa pasina utaratibu kufuatwa.

“Sisi ni kanisa huru linalojitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi lakini kilichotufikisha hapa ni kutokana na kufukuzwa kwa mchungaji ,askofu ametusababishia mgogoro mkubwa mapaka hatuna amani watu wa Makambako tunaomba serikali itusaidie,najua yupo waziri wa mambo ya ndani pia yuko msajili wa vyama atusaidie watu wanatumia katiba isivyo sahihi”alisema Besta Luvanda

Elia Joseph amesema“Sisi waumini hatuna mgogoro wowote na mchungaji wetu lakini yeye moja kwa moja amekuja kufukuza mchungaji wetu na sisi waumini hatukubaliani na ametuvurugia amani hapa tulipo”

Waumini hawa wameiomba serikali kuingilia kati ili kumaliza mgogoro huu huku wakieleza nia yao kuwa ni kuachana na ushirika huo pamoja na kurejeshewa mchungaji wao jambo ambalo mwenyekiti wa TFC anadaiwa kushindwa kulitekeleza.

Mwenyekiti wa TFC Askofu Godfrey Malasi anaetuhumiwa na waumini hao amesema

“Tulichoamua sasa tunaandika waraka wa amani kwamba wakitaka kuendelea pale waendelee wenyewe kama wanafikiri wana haki zote na sisi hatutawagusa tena ili wawe na amani lakini katika utaratibu wale watu walichokifanya sio sahihi na kwa kuwa wameamua kutukana sisi tumenyamaza Mungu ataamua mwenyewe”alisema Askofu Malasi

Aidha amesema kuwa kuna taasisi ambazo zipo nyuma ya jambo hilo wenye lengo la kumchafua Askofu na kuomba vyombo vya ulinzi kuchunguza watu hao.

Inadaiwa mgogoro huu ulifikishwa katika vyombo vya ulinzi na usalama wa raia,nimemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi wa polisi Khamis Issa ambae mapema hii leo amefika kanisani hapo na kuzungumza hatua walizozichukua.

“Hatua tulizochukua ni pamoja na kumshirikisha mkurugenzi wa mji na taasisi zingine zinazohusika na kutatua mgogoro na hapa tumekuta mabango yapatayo arobaini yakiwa yanapinga uamuzi wa askofu,tunawaomba uongozi wa juu wa hili kanisa wajaribu kulitafakari jambo hili na kuliangalia upya ili liweze kuleta amani katika mji wetu wa Makambako,na nishauri huu uongozi uliopo hapa kama hauleti uvunjifu wa amani wangeuacha tu uendelee”alisema Hamis Issa

Aidha ametoa wito kwa taasisi , na vikundi kuwa na uwazi katika mifumo ya uendeshaji wa taasisi zao ikiwa ni pamoja na kuweka bayana taratibu walizojiwekea.
Baadhi ya waumini wa kanisa la MCC wakiwa wamezingira gari iliyokuwa imembeba mchungaji mpya aliyefikishwa kwa ajili ya kuendesha kanisa hilo mara baada ya kuondolewa kwa mchungaji wa awali.

Waumini wa kanisa la MCC wakiwa wamebeba mabango nje ya kanisa kwa madai ya kupinga uamuzi wa Askofu wa kumuondosha mchungaji wa kanisa hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...