Na Amiri Kilagalila,Njombe
Hukumu ya kesi ya jinai namba 53 ya mwaka 2021 dhidi ya Anna Sanga (36) wa kijiji cha Lupalilo wilayani hapo pamoja na mwanafunzi wa shule ya msingi Lupalilo (13) walioshtakiwa kwa makosa ya wizi wa vitu mbalimbali, imetolewa.
Imeelezwa katika mahakama ya Wilaya ya Makete kuwa washtakiwa hao mnamo Septemba 4, 2021 majira ya saa 5 asubuhi mlalamikaji aitwaye Sara Sanga (50) aliibiwa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki 8 na elfu 85 ambavyo ni mali yake halali.
Hata hivyo upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wake dhidi ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Anna Sanga baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani pasipo shaka.
Mahakama hiyo imemhukumu mwanafunzi huyo wa shule ya msingi Lupalilo kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya shilingi 85,000 kwa mlalamikaji.
Hukumu hiyo imetolewa Novemba 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Makete Mh. Ivan Msaki pamoja na mwendesha mashtaka wa serikali Asifiwe Asajile.
Chanzo:Green fm Makete
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...