Charles James, Michuzi TV

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la PCI la Nchini Marekani imezindua muongozo wa kitaifa wa utoaji huduma ya chakula na lishe mashuleni.

Muongozo huo unalenga kuwaelekeza wasimamizi, watekelezaji na wadau namna bora ya kushiriki, kusimamia, kutekeleza na kuboresha utoaji huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi shuleni wa Elimumsingi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ametoa maagizo kwa Idara zote za Serikali na Wizara kusimamia utekelezaji huo kwani una tija kwa Taifa na wanafunzi nchini.

Dk Akwilapo pia ametoa rai kwa wadau wa elimu na wazazi kushiriki katika kuwapatia watoto vyakula wakiwa mashuleni kwani kufanya hivyo kunaongeza utimamu wa wanafunzi katika masomo.

" Lengo la uzinduzi wa muongozo huu ni kuufahamisha umma, watendaji Wakuu na wadau wote katika ngazi zote kuhusu uwepo wa muongozo unaoelekeza namna bora ya utoaji, usimamiaji na ufuatiliaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni. Uzinduzi huu unalenga kutoa hamasa kwa wadau mbalimbali kuona umuhimu wa kushiriki katika kutoa huduma ya chakula shuleni," Amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa PCI ambao ndio wawezeshaji wa mradi huo, Nicholas Fod ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliuonesha katika utekelezaji wa muongozo huo ambao umekua na mafanikio toka uanze kutekelezwa katika Mkoa wa Mara.

Amesema lengo la muongozo huo walianza nalo katika Mkoa wa Mara kwenye Halmashauri nne, Kata 45 na Shule 251.

" Mafanikio makubwa yamepatikana toka tuanze utekelezaji wa muongozo huu katika Mkoa wa Mara kwani tumeboresha maendeleo ya wanafunzi kutoka asilimia 80 mwaka 2017 hadi asilimia 89 mwaka 2019.

Ongezeko la wanafunzi wanaotumia lishe limefikia asilimia 84 kutoka asilimia 47 huku pia wanafunzi walioshindwa shule kwa sababu ya magonjwa wakipungua kutoka asilimia 6.3 hadi asilimia 3.9," Amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hudum za Jamii, Stanslaus Nyongo amepongeza juhudi za Serikali katika kuimarisha Afya ya akili ya wanafunzi huku akiahidi kwa niaba ya Wabunge wenzake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha muongozo huo.

" Tunampongeza Rais Samia kwa muongozo huu ambao naamini sasa unakwenda kuboresha Afya ya akili ya wanafunzi wetu, watoto wetu watasoma vizuri kwa sababu ya miundombinu inayowekwa na Serikali yetu lakini pia watakula vizuri.

Nitoe wito kwa viongozi wenzangu wakiwemo Wabunge na Madiwani kusimamia kidete utekelezaji wa muongozo huu na kuunga mkono, tuhamasishe na tusiwe wa kwanza kukwamisha," Amesema Nyongo..

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo akizungumza wakati akizindua muongozo wa kitaifa wa utoaji huduma ya chakula na lishe shuleni.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la PCI, Nicholas Fod ambaye Shirika hilo limeshirikiana na Serikali kuandaa muongozo wa kitaifa wa utoaji huduma ya chakula na lishe shuleni akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof James Shemdoe akizungumza kwenye uzinduzi wa muongozo wa kitaifa wa utoaji huduma ya chakula na lishe shuleni uliofanyika leo jijini Dodoma

Sehemu ya wanafunzi waliohudhuria uzinduzi wa muongozo wa kitaifa wa utoaji huduma ya chakula na lishe shuleni uliofanyika leo jijini Dodoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...