Mkurugenzi wa Huduma za ushirika TAEC Edgar Mbaganile akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano kwa watumishi 7 kutoka mtwara yaliyofanyika Jijini Arusha kwenye Ukumbi wa TAEC
Salehe Mikidad mkuu wa uhifadhi vyanzo vya mionzi :Tume h imeamua kujikita kwenye kutoa elimu kwa jamii na kwa wataalam wanaotumia vyombo vya mionzi maeneo ya kazi ili waweze kuvitunza vizuri na kuepusha madahara
Washiriki wa mafunzo ya kujengewa uelewa kutoka mtwara wakimsikiliza kinachoendele kabla ya kukabidhiwa vyeti ya kubitimu mafunzo hayo
Na.Vero Ignatus
Tume ya Nguvu za Atomiki nchini Tanzania (TAEC) imesema kuwa yapo madhara yanayoweza kujitokeza kama vyanzo vya mionzi vitatumika ndivyo isivyo kwaajili ya salama .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Ushirika TAEC Edger Mbaganile kwamba tume hivyo imeamua kujikita kwenye kutoa elimu kwa jamii na kwa wataalam wanaotumia vyombo vya mionzi maeneo ya kazi ili waweze kuvitunza vizuri na kuepusha madahara yanayoweza kuepukika
Akifunga mafunzo ya siku tano yaliyofanyika katika makao makuu ya TAEC Jijini Arusha mwishoni mwa wiki Ijumaa ya Tarehe 29 Octoba 2021, Mbaganile alisema kuwa watumishi 7 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Mtwara amewataka kuzingatia kile walichokipata katika mafunzo hayo, kuhakikisha wanajikinga na kuwakinga wananchi dhidi ya madhara yatokanayo na mionzi.
Aidha wataalamu hao wamesema kwa elimu waliyoipata wanaweza kutambua viwango vya mionzi, ambavyo si salama kwa wafanyakazi katika maeneo ya kazi, ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mionzi, ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za usalama wa mionzi mahala pa kazi , bila kusahau kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa inayoelekeza namna salama ya matumizi ya mionzi.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao walionufaika na mafunzo hayo ya siku 5 kutoka TPDC Mhandisi Ally Chemba, alisema kuwa kabla ya kupata mafunzo alikuwa hawana uelewa wowote juu ya mionzi,kwani yeye binafsi yupo kwenye mitambo ya kuchakata gesi mtwara,na huwa anafanya matengenezo ya vifaa hivyo vyenye mionzi ,hivyo yatamsaidia namna ya kujikinga na kuepusha madhara kwa wengine
Pale kwetu mtwara kuna vifaa vyenye vyanzo vya mionzi kuna wageni mbalimbali wanakuja kujifunza mambo mbalimbali,hata vifaa vya ukaguzi vina vyanzo vya mionzi tumefunzwa vyema namna ya kuikinga jamiii haswa wale wanaotute,mbelea wasipate athari za mionzi.Alisema Ally.
Amesema kuwa wamepatiwa mafunzo namna ya kutambua vyanzo mbalimbali vya mionzi na kuvipima, hivyo wameahidi kwenda kufanya maboresho makubwa kuhakikisha kwamba wale wananchi wanaowatembelea kiuwandani,kutoka salama bila kudhurika na usimamiaji wa afya za wafanyakazi kwenye maeneo yao ,mazingira pamoja na usalama wa mitambo,bali baada ya mafunzo amempa uelewa mkubwa kwenye masuala ya mionzi
‘’Sisi kwenye eneo letu la kazi tuna kile kifaa cha kukagulia mizigo inayokuja kwenye maeneo yetu amayo kwa mafunzo haya tumeshajua kwamba ni chanzo cha mionzi lakini tunawezaje kuwa na chanzo cha mionzi na tukabakia salama ndio mafunzo haya yamejikita huko,sambamba na kuangalia mizigo inayokuja haina vihatarishi vyovyote’’.alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...