Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

SHIRIKA la Bima Visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom wafanya Uzinduzi wa huduma za bima (Vodabima)kwa njia ya kidigitali.

Akizungumza hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Araf Haji amesema Ushirikiano huo pamoja na wadau wengine kama Shirika la posta nchini umesaidia shirika la bima (ZIC) kujitanua zaidi katika Maeneo mbalimbali ya nchi ambapo Hadi sasa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) limekuwa na  matawi kila Kona ya nchi .

"Tumetoboa nchi nzima na imejengeka Imani kubwa kwa Wateja wetu kuwa ni Miongoni mwa Shirika lenye ukuaji mkubwa hapa nchini Hali ambayo imekuwa ikituwezesha kubuni huduma bora na rafiki za kibima ili Kulinda n kurejesha Imani kwa Wateja wetu.

Aidha, Haji ameeleza kwa namna Ushirikiano huo wa huduma ya kidigitali ya vodabima itakayowezesha wateja wao kupata huduma ya bima kwa kupitia M_pesa .

"Wateja wetu wataweza kupata huduma za bima kwa njia ya kidigitali yani vodabima kwa njia ya M_pesa ."

Pia ameongezea kuwa wana imani na vodabima ambayo inatumia Miundombinu ya teknolojia ya M_pesa na mtandao mpana wa Vodacom ambayo inapatikana katika maduka ya Vodacom nchini kote.

"Tunakwenda kuwafika Wateja wetu kwa urahisi zaidi huku tukiwahakikishia usalama zaidi katika utoaji wa huduma zetu za kibima."

Hata hivyo amesema Ushirikiano huo umekuja wakati muafaka kutokana na kudhamiria kwao kama Shirika kuongeza wigo wa mtandao wa utoaji huduma kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya kidigitali.

"Serikali imetoa Maelekezo hasa kwa Mashirika ya bima kuhakikisha huduma ya bima kwa wananchi walioko vijijini wananufaika zaidi kwani watakua kwenye nafasi ya kuweza kufahamu kwa kina na kwa urahisi huduma mbalimbali za bima zinazotolewa sokoni na Shirika letu."

Mkurugenzi Mtendaji Arafat Haji akizungumza na Waandishi Wahabari pamoja na wafanyakazi na viongozi kutoka Shirika la bima Zanzibar (ZIC) pamoja Kampuni ya Vodacom ambao wamezindua rasmi huduma ya kidigitali ya vodabima
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Said Basleym akifatilia kwa makini Uzinduzi huo unaolenga kuwafikia Wateja zaidi hususani wa vijijini

Picha ya pamoja baina ya Shirika la bima Zanzibar (ZIC) wakiwa pamoja na Kampuni ya Vodacom ikiwa sehemu ya Uzinduzi wa huduma ya kidigitali ya bima (Vodabima) ambapo imezinduliwa mapema Leo Visiwani Zanzibar


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...