Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
VIJANA nchini wameaswa kujitokeza kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara hususani fursa za kujitolea kukuza Maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na Michuzi Tv,Mara baada ya kutoa Mafunzo hayo Mkufunzi kutoka Umoja wa Mataifa (UN) Penina Nguma amesema Ni vizuri Vijana hususani wanafunzi Katika vyuo Vikuu kujijengea uwezo wa kujikita kujitokeza kwenye fursa mbalimbali zinazotolewa na Makampuni,Taasisi,Jumuiya,Mashirika au watu binafsi kwani zinawajengea uwezo wa kutafuta ajira, kutafuta Masoko kutokana na mikusanyiko au watu wanaokutana nao katika fursa hizo za kujitolea.
"Wasitazame nafasi walizonazo au hata vyeo vyao lakini wajitolee kwa lengo la kuimarisha na kuboresha Maendeleo yetu nchini kwa Mustakabali wa Taifa kwa ujumla bila Kujali maslahi."
Hata hivyo Nguma ameongeza kuwa wanafunzi Katika vyuo Vikuu waweze kukimbilia fursa za kujitolea hata kama hakuna faida za awali wanazopata ila kadri wanavyoweza kujitangaza na kufanya kazi Kwa bidii wataweza kunufaika na kuyaona Matunda kwa siku za baadae.
Nae Rais wa Chuo Kikuu Cha Zanzibar (SUZASO) Sleyum Abdallah amepongeza uongozi wa Umoja wa Mataifa UN kwa kutoa Mafunzo kwa wanafunzi wa chuo hicho.
"Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu katika Majukumu yao".
Abdallah amefafanua faida walizopata katika Mafunzo hayo ikiwemo kufuta taswira iliyojengeka hapo awali kuwa katika fursa za kujitolea hakuna faida yoyote badala yake fursa hizo zinalenga kumjengea umakini pamoja na kukuza mtandao kwa watu mbalimbali.
Nae Mmoja ya viongozi wanufaika wa Mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku 1 katika Chuo kikuu Cha Zanzibar kwa viongozi 24, Salum Ally amesema kupitia Mafunzo hayo Vijana wengi wataweza kujijengea uaminifu,uadilifu na Moyo wa kujitolea katika kazi zozote zile.
Picha ya pamoja baina ya Mkufunzi wa Mafunzo ya fursa mbalimbali za kujitolea kutoka Umoja wa Mataifa (UN) Penina Nguma pamoja na wanufaika wa Mafunzo hayo viongozi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZASO)Mkufunzi wa Mafunzo ya fursa za kujitolea kutoka Umoja wa Mataifa (UN) Penina Nguma akisikiliza kwa makini Mawasilisho ya viongozi kutoka Chuo Kikuu Zanzibar (SUZASO) wanufaika wa Mafunzo yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini kuhusu vijana kuzikimbilia fursa ambalimbali zinazotolewa na Makampuni,Taasisi Jumuiya ,Mashirika kwa lengo la kukuza Maendeleo ya Taifa


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...