Na.Khadija Seif, Michuzi TV
VIJANA wameaswa kutoshiriki ngono zembe na kujikita zaidi kupata Elimu ya Afya ya uzazi ili kutimiza Malengo yao wakiwa na Afya njema na Kupanga Familia Bora.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dkt international Kelvin Hudson amesema Vijana Kwa Sasa ndio wanaongoza Kwa kufanya ngono zembe nakupelekea kuingia kwenye namba kubwa ya watu wanaopata Maambukizi ya magonjwa ya zinaa hasa virusi vya ukimwi (HIV) hivyo kupitia Kampeni ya uhamasishaji masuala ya Virusi vya ukimu (VVU.) Kupitia Mchezo wa Baiskel Kwa siku tatu mfululizo katika fukwe za Visiwa vya Zanzibar.
"Taasisi yetu inalenga kupiga vita ngono zembe hususani Kwa vijana na Kampeni yetu mpya (Cycle for HIV) inalenga kukuza uhamasishaji wa masuala ya Virusi vya ukimu(VVU) Elimu karibu na kushirikisha Michezo Kwa Vijana Ili kuona Kwa jinsi gani vijana wananusurika na Magonjwa ya zinaa na kutumia Kinga na Kupanga familia Bora".
ameongeza kuwa Kwa kupitia Kampuni hiyo inayosambaza Vifaa tiba ikiwemo Kinga pamoja na vidonge vya kupanga uzazi kwa sasa imeteua Mabalozi ambao ni watu wenye ushawihi katika jamii kuona Kwa jinsi gani wataweza kutoa Elimu Kwa jamii ya kujikinga na Magonjwa ya zinaa .
Pia Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko DKT, Farida Rubanza amesema Kampeni hiyo itahusisha Mchezo wa kuendesha Baiskel katika fukwe za Nungwi Visiwani Zanzibar na hatimae kupatikana Mshindi ambae atapewa nafasi ya kula Bata na Mabalozi Yao.
"Calisah ni Mwanamitindo pamoja na Msanii ana Mashabiki wengi hivyo basi tumemteua kuwa Balozi wetu wa bidhaa ya bullcondoms,akifatiwa na Maggie,Tahiya pamoja na Djklaxx"
Balozi huyo mpya katika Kampeni hiyo Calisah amewasihi Vijana Kutunza Afya zao na kuhakikisha wanajikinga na Magonjwa ya zinaa kama vile gono,kaswende,ukimwi na mengine.
Balozi wa Kampeni ya uhamasishaji masuala ya Virusi vya Ukimwi (VVU) Calisah akiwahimiza vijana kutojihusisha na ngono zembe badala yake watumie Kinga pamoja na Kupanga uzazi Kwa ajili ya kuboresha Afya ya uzazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...