Na Mwandishi Wetu, Arusha.


TAASISI ya Elimu Tanzania (TET), imewasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu katika Mkutano Mkuu wa Maafisa  Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDEOA).

Mkutano huo ulioanza Januari 24 na kufikia tamati mapema jana Januari 28, katika ukumbi wa Lush Garden  Jijini hapa,  ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba aliwasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala hiyo ya Elimu.

Mitaala hiyo ni pamoja na Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu.

Baada ya wasilisho hilo la Dkt. Komba, Maafisa Elimu hao walipata nafasi ya kupitia na kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa Mitaala hiyo.

Mkutano huo wenye kauli mbiu ya; "Kuboresha miundombinu ya Shule na kuimarisha Elimu kwa Maendeleo Endelevu na kukuza uchumi wa Taifa"

Zoezi hili la ukusanyaji wa maoni linatarajiwa kukamilika tarehe 31/01/2022 ambapo mchakato wa kuboresha Mitaala itachukua muda wa miaka 3 na Mitaala mipya inatarajiwa kuwa darasani mwaka 2025.


 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania  (TET), Dkt. Aneth Komba akiwasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala kwa Maafisa wa Elimu Mikoa na Halmashauri (REDEOA). Katika mkutano uliofanyika jana Januari 28,2022 katika ukumbi wa Lush Garden Jijini Arusha.

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri  nchini (REDEOA) wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jana Januari 28,2022 katika ukumbi wa Lush Garden Jijini Arusha


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...