Na. John Mapepele

Serikali tayari imetenga shule 56 za michezo nchi nzima ili kuibua na kukuza vipaji vya michezo kwa watoto nchi nzima.

Kauli hii imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  Februari 4, 2022 katika ubalozi wa China jijini Dar es Salaam kwenye siku ya mwaka mpya wa Taifa hilo na siku ya uzinduzi wa mashindano ya mwaka 2022 ya Olympiki ya Beijing ya majira ya baridi.

Utengaji wa shule hizo pia ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati akifungua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Juni 8, 2021 ambapo alielekeza  Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na mambo mengine isimamie utengaji wa shule maalum za Michezo nchi nzima.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba kutenga kwa shule hizo za michezo  nchi nzima ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi Chama cha Mapinduzi (CCM) unaoitaka Serikali kuibua vipaji vya watoto ili kupata wanamichezo bora na kuimarisha michezo kwa ujumla.

Aidha, amesema hadi sasa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara   ya TAMISEMI na Wizara yenye dhamana ya Elimu zimesha ainisha shule hizo kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya miundombinu ya michezo.

Ameongeza kuwa Wizara yake itahakikisha inasimamia zoezi hili kikamilifu ili kuleta Mapinduzi makubwa kwenye michezo.

Amemwomba  Balozi wa China nchini Chen kuiomba Serikali yake kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya michezo ya shule hizo ili Ilani ya CCM ambayo inaendana na ile ya Chama cha CPC cha nchini China iweze kutekelezwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...