Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kifungo cha nje miezi 12, mzee Malima Para (69) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka moja la kumuua Michael Shadrack bila ya kukusudia kwa kumkata na panga tumboni na shingoni.
Hukumu hiyo imesomwa leo Machi 8, 2022 na Jaji Edwin Kakolaki baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo.
Hata hivyo kabla ya kusomwa kwa adhabu, Jamuhuri iliomba mshtakiwa kupewa adhabu kwa mujibu wa sheria.
Akijitetea mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa yeye ni mkosaji wa kwanza pia amekaa gerezani kwa muda mrefu na sasa anaumwa TB na ana mri wa miaka 69 na anafamilia inayomtegemea ana mke na watoto sita
Akisoma adhabu hiyo Jaji Kakolaki amesema amezingatia maelezo ya pande zote mbili, wa utetezi na Jamuhuri na kwamba ni ukweli kwamba mauaji yaliyofanywa na mshtakiwa Para yalikuwa siyo ya kukusudia bali yalitokana na ugomvi uliochangiwa na marehemu mwenyewe.
Amesema, pia mahakama imetilia maanani maombi yaliyotolewa na wakili wa Mshtakiwa kuwa mteja wake ni mkosaji wa mara ya kwanza, ameisjakaa gerezani kwa zaidi ya miaka minne na pia ni ana Umri mkubwa
Ni kweli mshtakiwa ana umri mkubwa sasa angekuwa anafurahia maisha ya uzeeni, lakini pia kupitia kitendo cha mshtakiwa mtu aliuawa na mtu uyo alikuwa na haki ya Kuishi.
"Adhabu inayotolewa na mahakama inabidi kumfanya mtu arekebishe tabia na kufikisha ujumbe kwa jamii, Mahakama Inaona Kuwa kifungo cha jela haitampa funzo huu hivyo mahakama inakupa kifungo cha nje na hatatakiwa kufanya kosa lolote la Jinai hata ndani ya Miezi 12 hata liwe dogo kiasi gani.
Mapema, katika maelezo ya kosa imedaiwa, Desemba 14, 2017 mshatakiwa pamoja na marehemu ambao walikuwa wakifahamiana na walikuwa wanaishi eneo la makondeko wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani walikutana katika mi msitu wa Chamamgwe Bagamoyo Pwani.
Imeelezwa wakati wanakutana siku hiyo wote wawili walikuwa na Mbwa wanaowafuga, lakini wakiwa msituni hapo marehemu alianza kuwashambulia mbwa wa mshtakiwa kwa kuwapiga.
Imeelezwa, mshtakiwa alikasirishwa na kitendo kile na kuchukua panga lake na kumpiga marehemu shingoni ma tumboni kisha akaondoka eneo hilo na kumuacha marehemu msituni.
Desemba 15,2017 taarifa za Kutokuonekana kwa marehemu zilitolewa kituo cha Polisi Bagamoyo hivyo wanakijiji walianza msako wa kumtafuta marehemu ambapo baadae jioni walifanikiwa kuuona mwili wa marehemu katika msitu huo.
Polisi na daktari walifika eneo la tukio na mwili wa marehemu ulipochunguzwa ulionyesha kuwa kifo chake kimesababishwa na majeraha kuvuja damu fuja damu nyingi ambazo zilisababishwa na Kupigwa na kitu chenye Nja kali.
Katika kesi hiyo inadaiwa, Desemba 14,2022 Huko Bagamoyo katika eneo la Chamangwa, mshtakiwa Para alimuua bila kukusudia Michael Shadrack.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...