WANAWAKE Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) washeherekea siku ya wanawake na watoto wa kituo cha Kulelea watoto cha UMRA kilichopo Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa kukabidhi msaada wa Vitu mbalimbali katika kituo hicho, Mwanyekiti wa Kamati ya Wanawake Tanesco Makao Makuu, Prisca Maziwa amesema kuwa msaada huo ni nguvu za pamoja za Shirika hilo.

Amesema ikiwa ni kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake wameona kusheherekea pamoja na watoto wa kituo cha MRA ili watoto hao waonje upendo wa mama ingawa wao hawana wazazi.

"Sisi tupo karibu na jamii na leo tumekuja kuwatembelea watoto wetu na kuwaletea mahitaji yatakayowasaidia katika kwa muda kidogo." Amesema Prisca.

Hata hivyo amewashukuru wafanyakazi wa Tanesco kwa kufanikisha kupata vitu mbalimbali kwaajili ya watoto yatima.

Prisca ametoa wito kwa watu binafsi mashirika, taasisi mbalimbali kujitoa kwaajili ya watoto wenye mahitaji na kutowaachia watu wachache kuwalea watoto hao.

Wafanyakazi wa Tanesco wanawake makao makuu wamewawakilisha pia wanawake wa vituo vya kufua Umeme na kampuni Tanzu za Tanesco, wamewasilisha katika kituo cha UMRA vitu mbalimbali ikiwemo Mchere, sukari, Mafuta, Maharage, Chumvi, Sabuni na vitu ambavyo vinatumika kijamii.

"Kadiri Mungu anavyokujalia toa kwenye kituo hicho au vituo vingine kusaidia katika mahitaji mhimu ya binadamu na kutoa faraja na Upendo kwa watoto hawa." Amemalizia Prisca.

Kwa upande wake Mwasisi wa UMRA Orphanage Centre, Rahma Kishumba amewashukuru wafanyakazi wa Tanesco kwa kutoa misaada mbalimbali kwa kuweza kuwasaidia ulezi wa watoto.

"Sinabudi ya kusema wakinamama wa Tanesco Mungu awajalie na awalipe na kila rakheri na shukrani kwa Mkurugenzi wa Tanesco." Amesema Bi Rahma.

Kwa upande wa Mwakilishi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha UMRA, Abrakim Mohamed amewashukuru wafanyakazi wanawake wa Tanasco na kuwaombea yote mema.




Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiwa na watoto wa Kituo cha kulelea watoto Yaztima kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam le Machi 8, 2022 ikiwa ni kusheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwanyekiti wa Kamati ya Wanawake Tanesco Makao Makuu, Prisca Maziwa akimkabidhi mtungi wa Gesi Mwasisi wa UMRA Orphanage Centre, Rahma Kishumba leo Machi 8,2022.

Baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco wakitoa vinywaji kwa watoto wa Kituo cha UMRA kilihopo Magomeni jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...