Janeth Raphael - Dodoma

Waziri wa Maji jumaa Aweso amekerwa na baadhi ya viongozi wa wizara hiyo wanaofanya kazi kwa dili na baadhi ya wakandarasi hali amabayo ameitaja kuwa ni kichocheo cha rushwa wakati serikali inakemea vitendo hivyo.

Aweso ameyasema hayo  jijini Dodoma  mara baada yakukutana na wadau wa sekta ya maji Tanzania na viongozi wa sekta hiyo  ambapo alionyesha kuchoka kuona baadhi ya ofisi za wizara hiyo zinaongozwa kidalali hali inayopelekea kero kwa watu wenye nia njema ya kusaidia upatikanji wa nishati ya maji kwa wananchi.

Aweso amewataka watumishi wa sekta ya maji kuacha ubabe na badala yake kuheshimiana kwasababu wao na wadau wengine wa sekta hiyo wanategemeana kufanikisha malengo ya Serikali.

Ubabe tuachane nao tuheshimiane kwasababu wote tunategemeana, hatutegemei hilo kufanywa katika sekta ya maji,”amesema Aweso.

Katika hatua nyingine  Aweso amesema kila kiongozi awe na uchungu unaowakuta wananchi pindi wanapokosa huduma maji safi na salama na hiyo iwe moja ya kujipima wenyewe katika utendaji kazi wao, huku baadhi ya washiriki wakitoa kero zao ikiwa ni pamoja na mizunguko wanayokutana nayo maofisini pindi wanapotafuta vibali na baadhi kucheleweshewa malipo yao ya kandarasi.

Amesema changamoto kubwa ya baadhi ya makandarasi ni uongo ambapo wanapoulizwa kwanini wamechelewesha kazi hutoa visingizio vya uongo.

Aidha, Aweso amesema Rais Samia Suluhu Hassan atakutana na wadau wote wa sekta ya maji ambao mkutano huo utamuhusisha pia Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Amesema mkutano huo utafanyika jijini Dar es Salaam Machi 22, mwaka huu.

Pia amesema Serikali imetoa Sh41 bilioni kwa ajili ya kulipa makandarasi na kuwataka watendaji wa sekta hiyo kulipa madeni yote wanayodaiwa.

Hata hivyo, Aweso amesema suala la uaminifu linaumuhimu mkubwa na kutoa mfano wa mmoja wa makandarasi Wilaya ya Handeni ambaye alilipwa Sh600 milioni lakini hakufanya kazi.

Amesema alipoulizwa kwanini hafanyi kazi, mkandarasi huyo alisema kuwa ni kwasababu kuna wachawi.

Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa), John Msengi amesema makandarasi wazawa wengi hawana mitaji na ndio maana wengi wao hata wakipewa malipo ya awali yanaisha kabla ya kumaliza shughuli iliyokusudiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa, Clement Kivegalo amesema wako mbioni kutengeneza mfumo wa Tehama ambao utawezesha wakandarasi kujaza vyeti vya malipo (certificate) kwa kutimia mtandao na hivyo kurahisisha utendaji.

Naye Mwakilishi wa makandarasi, Jumanne Werema amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili makandarasi nchini ni ucheleweshaji wa malipo, ucheleweshaji wa misamaha ya kodi la Ongezeko la Thamani (VAT) na mikataba kutokuwa wazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Anthony Sanga amesema wamechukua maoni na ushauri wao na kwamba watafanyia kazi na kuwajibu kwa maandishi.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso , akizungumza na Wadau wa Maji katika kikao Maalum cha wadau hao Dodoma
Baadhi ya Wadau wa Maji wakimsikiliza Waziri wa Maji ,Jumaa Aweso katika kikao maalum Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...