Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ) kanda ya kaskazini , Imelda Salum (wa kwanza kushoto) akikabidhi leseni kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAVVY MEDIA GROUP LTD inayomiliki SAVVY FM 105.3 ARUSHA Awaichi Mawalla….Tukio hilo limeshuhudiwa na Mkurugenzi Uendeshaji wa SAVVY Media Group LTD, Grace D. Maleto na Mhariri Mtendaji wa SAVVY MEDIA GROUP, Baraka Sunga .Tukio hili limefanyika leo katika ofisi za Mamlaka jijini Arusha.



Wanawake wa nguvu katika picha ya Pamoja wakiikumbusha Jamii kuondoa Upendeleo wenye ubaguzi/ukandamizaji hasa wanawake. Pichani ni Wanawake wa Shoka toka kushoto ni Secilia Mkoba ambaye ni Mchambuzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania –Masuala ya kifedha, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ) Kanda ya Kaskazini Eng. Imelda Salum, Mkurugenzi Mtendaji wa SAVVY MEDIA GROUP LTD inayomiliki SAVVY FM 105.3 ARUSHA bi Awaichi Mawalla na Mkurugenzi Uendeshaji wa SAVVY Media Group bi Grace D. Maleto.



Maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Kaskazini (toka kushoto ni Abel John, Peter Omao, Eng. Jan Kaaya na Julius Felix ambaye ni wa pili toka kulia) wakiongozwa na Meneja wa (TCRA ) Kanda ya Kaskazini Eng. Imelda Salum mwenye vazi jeusi lenye mabaka mekundu sambamba na Wakurugenzi wa SAVVY MEDIA GROUP baada ya makabidhiano ya Leseni katika ofisi ya TCRA Kanda ya Kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...