Na Abdullatif Yunus - Michuzi Kagera.
Wakati Duniani ikiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 08, kila Mwaka, Wafanyakazi wa Kike kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) wametumia nafasi hiyo kutembelea Kituo cha Kulelea Watoto wadogo cha Ntoma Maruku na kuwashika mkono.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi walizoambatana nazo Meneja uhusiano wa Mamlaka hiyo Julieth Shangari amesema, kama BUWASA wamewiwa kufika Kituoni hapo kutoa Zawadi hizo kwa Walezi na watoto hao wadogo, waliopatikana kwa namna mbalimbali wengine ikiwa na sababu za mama zao kufariki baada kujifungua, wengine wakitupwa na mama zao baada ya kujifungua na wengine wakikimbiwa na wazazi kufuatia migogoro mbalimbali ya kifamilia.
Julieth amekaririwa akisema "Siku hii ya wanawake BUWASA tumeamua kushinda hapa, tumepika chakula wenyewe na kula pamoja na watoto hawa ili wafurahi nasi tunaposherehekea siku yetu, lakini ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wateja wetu ambao wanatumia huduma ya Maji.." amesema Julieth.
Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na mchele, sukari, mafuta ya kula, viatu, sabuni mafuta ya kupaka, chumvi, soda, juisi na maji. Kituo hicho cha kulea watoto mpaka sasa kipo chini ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi kikiwa na jumla ya watoto 39 wenye umri kuanzia Mwezi mmoja mpaka Miaka miwili na miezi mitatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...