IKIWA Dunia inaadhimisha siku ya Wanawake Duniani, Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka nchini(DART) umetoa msaada wa vifaa, mahitaji mbalimbali zikiwemo shuka pamoja na kuchangia damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mloganzila iliyopo Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam.
Wakikabidhi msaada huo leo, DART kwa kushirikiana Wakala wa utoaji huduma za Mabasi ya Haraka (UDART) wameeleza lengo lao ni kusaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wagonjwa wanaopatiwa huduma mahali hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa DART, Kaimu Mkuu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu DART Dkt. Eng. Philemon Mzee, amesema wametoa msaada huo kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani wakiwaunga mkono wanawake wa taasisi hiyo.
"Kwa pamoja sisi na wenzetu wa UDART tuliona vyema kuja kuwafariji kwa kiasi kidogo wagonjwa waliolazwa hospitalini hapa wakiwemo aakina Mama, tupo hawa kuwafariji wakati huu wanapopata matibabu hospitalini hapa" alisema Mzee.
Amesema, wamekuwa wakiboresha huduma ya usafiri katika hospitali hiyo kwa kuhakikisha kunakuwa na usafiri kwa kila baada ya dakika ishirini ili kuwasafirisha wananchi wanaokwenda kutibiwa na kuwaona wagonjwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa UDART Zaitun Hassa amesema wanatambua mchango mzuri hususani wa utoaji wa huduma kutoka katika hospitalini hao na kuongeza kuwa msaada walioutoa ni kutambua juhudi za hospitali hiyo sambamba na kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
Bi. Zaitun ametumia wasaa huo kuwashauri watanzania kushiriki Sensa ya watu ya makazi itakayofanyika mwaka huu amewataka ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango sahihi ya maendeleo na kueleza kuwa wameendelea kutoa huduma ya usafiri katika hospitali hiyo kadri ya uhitaji kwa kuanza na mabasi manne ambayo huingia hospitalini hapo kila baada ya dakika 20.
Aidha aliwaomba wadau wengine zikiwemo taasisi mbalimbali kujitokeza kutoa misaada mbalimbali hospitalini hapo kutokana na mahitaji mbalimbali yaliyopo kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo ya Mloganzila Dkt. Julieth Magande, mbali na kuwashukuru watoa huduma hao wa mabasi yaendayo haraka kwa msaada huo, alisema Mloganzila kama ilivyo hospitali zingine wanakabiliwa na changamoto ya mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha utoaji huduma.
Alisema Dkt. Magande wakiwa kama wasimazi wa huduma za hospitali hiyo kwa kiasi fulani bado wanahitaji misaada ya kila aina yakiwemo mashuka na mengineyo ili kuwawezesha wagonjwa kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa.
Mbali na kuchangia damu vifaa viilivyotolewa na DART ni pamoja na shuka 50, kandambili, dawa za meno, mafuta ya kupaka, sabauni za kufulia na kuogea.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila Dkt. Julieth Magande akizungumza mara baada ya kuupokea ugeni huo na kueleza kuwa wakala hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero ya usafiri kwa wagonjwa wanaokwenda kutibiwa hospitalini hapo, Leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...