Yasema mengi yamefanyika, yaahidi makubwa zaidi.

Na Grace Semfuko MAELEZO.

Machi 10, 2022.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini-DCEA, katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, imedhibiti uingizwaji wa tani 120.5 za kemikali bashirifu aina ya yabisi, pamoja na lita 40 za kemikali hiyo aina ya kimiminika ambazo zilikuwa zikiingizwa Nchini.

Mamlaka hiyo katika kipindi hicho pia, iliweza kukamata Wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya 11,716 ambao walidaiwa kukutwa na kilo 35, 227. 25 za dawa za aina mbalimbali.

Akitoa taarifa ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Madarakani, Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya, amesema pia wameteketeza ekari 185 za mashamba ya bangi katika maeneo mbalimbali nchini, na mashamba ya Mirungi ekari 10 ambapo katika zoezi hilo, wapo watuhumiwa waliofikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea kusikilizwa.

"Katika kipindi hicho jumla ya watuhumiwa 100 walikutwa na dawa aina ya Cocaine, lakini pia katika kipindi hicho watuhumiwa 588 walikamatwa wakiwa wanajihusisha na biashara na utumiaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin, watuhumiwa 9,484 walikamatwa wakijihusisha na Dawa za kulevya aina ya bangi, watuhumiwa 1,395 walikutwa wafitumia na kufanya biashara ya mirungi, katika kipindi hicho mashamba 132 ya watuhumiwa 132 wa mashamba ya bangi walikamatwa na watuhumiwa wawili wa mashamba ya bangi walikamatwa" amesema Kashna Jenerali Kusaya.

Kusaya amesema kufuatia Tanzania kufanya vizuri kwenye udhibiti wa kemikali hizo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya na uhalifu-UNODC imeiteua Tanzania kuwa nchi kinara katika udhibiti wa kemikali bashirifu, na kuipa jukumu la kutoa elimu kuhusu udhibiti wake katika nchi tisa Barani Afrika.

"Watanzania wenzangu, kuutokana na Taasisi yenu kufanya vizuri sana kwenye udhibiti wa dawa bashirifu, ofisi ya umoja wa mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya na uhalifu UNODC imeiteua Tanzania kutoa elimu kuhusu udhibiti huo kwa nchi za Rwanda, Burundi, Madagascar, Zambia, Malawi, Ethiopia, Msumbiji, Elitrea na Mauritius" amesema Kusaya.

Aidha amebainisha kuwa DCEA kwa kushirikiana na taasisi na za Serikali za Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bohari ya Dawa- MSD na Bodi ya kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya wanasaidiana katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali bashirifu, ili kuondokana na dawa za kulevya ambapo wameanzisha mradi wa ushirikiano Kati ya Serikali na taasisi 27 za kemikali hiyo, na vyama viwili vya dawa za binaadamu, ambapo wametia saini mkataba wa makubaliano ya udhibiti huo.


Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...