Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Kata ya Terati ,Halmashauri ya my ya Jiji la Arusha alipoenda kutembelea mradi wa mabwawa 18 ya Kutibu maji Taka.Picha na Vero Ignatus.

Mwonekano wa baadhi ya mabwawa Kati ya 18 yaliyopo kata ya Terati,ambayo Mhe.Mpango ameshauri yachujwe na kubadilishwa matumizi kwaajili ya kilimo na umwagiliaji.Picha na Vero Ignatus




Na Vero Ignatus,ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ametembelea mradi wa mabwawa 18 ya kutibu maji taka yaliyopo kata ya Terati Mkoani Arusha uliogharimu kiasi Cha tsh 39.8 bilioni ambao ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa bil 520.

Ameyasema hayo Leo wakati alipotembelea mradi wa mabwawa hayo,unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira( Auwsa) ambapo alishauri maji hayo yachujwe kwaajili ya kubadilisha matumizi, kwaajili ya kilimo na umwagiliaji katika eneo hilo lenye ukubwa hekari 250 mradi huo ulipo.


Mhe.Mpango amesema Novemba mwaka jana alitembelea nchini Israel Jiji la telaviv na alijionea jinsi walivyobadilisha eneo la jangwa kuwa la kilimo kwa kutumia Teknolojia ya maji taka ,ambapo mazingira yamebadilika na siyo jangwa tena

"Mwaka Jana Mimi nilipata fursa ya Isarael nilienda hadi Jiji la Telaviv ambalo ni jangwa na maji taka yote yanachujwa yanaenda kumwagilia jangwa na limebadilika sasa hakuna jangwa tena na limekuwa la kilimo,"alisema

Alisema kama wao wanaweza hilo alishauri Jiji kuangalia jinsi ya kutumia wataalamu kuhakikisha maji hayo hayapotei yatumike kwenye uzalishaji kwenye eneo la ekari 250 ambalo kame badala ya kurudisha mtoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Justine Rujomba Alisema kukamilika kwa mabwawa hayo kumesaidia kuongeza uwezo wa katibu maji toka lita milioni 3.5 ya mabwawa ya zamani hadi kufikia lita zaidi ya milioni 22.

Mhandisi Rujomba alisema kuwa Mfumo huu umesaidia uongezaji wa uondoaji wa maji taka kwa asilimia 7.6 na kufikia asilimia 30%ambapo mbali na ujenzi wa mabwawa hayo, kumejengwa nyumba za wafanyakazi, matundu ya vyoo 144 kwenye shule 25 na maabara.

Mhandisi Rujomba alisema kuwa Kuhusu kutumia maji hayo kwenye uzalishaji wapo kwenye hatua za awali za mazungumzo na Jiji pamoja na Mbunge kwani wapo wananchi wanaohitaji maji hayo kwa ajili ya matumizi mengine.


Akijibu ombi la wananchi wa Kata ya mkono juu ya gari la wagonjwa,bima ya Afya,nyaya za umeme na Barabara Mhe.Mpango amesema kuwa Serikali inaendelea kushughulika na suala la bima ya Afya ,hususani kwa wazee maana limekuwa na changamoto,huku barabara kiwango cha lami aliiagiza Tarura kuangalia bajeti yao, ili kuiboresha barabara hiyo iwe ya chagarawe au kiwango cha lami

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...