Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedaha na Mipango Bi. Amina Shaabani ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kikao cha kamati ya fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ajenda zilizojadilliwa katika kikao hicho ni pamoja na kuidhinishwa kwa bajeti ya kutafsiri kwa Kiswahili vitabu vilivyoandikwa na Hashim Mbitta kuhusu harakati za ukombozi kusini mwa Afrika na ujenzi wa sanamu ya kumbukumbu ya Hayati Julius Nyerere ili kuenzi mchango wake katika ukombozina maendeleo katika kanda ya nchi za SADC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...