SERIKALI kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imewezesha kulipa madeni yenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 175 kwa wazabuni waliotoa huduma mbalimbali kwenye Wizara hiyo na Taasisi zake.

Hayo yamesemwa leo  na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Lawrence Tax wakati akiwasilisha mafanikio ya kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Dk Stergomena amesema kuwa kuwezeshwa huko kwa Wizara yake kulipa madeni hayo kumejenga imani kwa Serikali na kuwezesha Wizara kuendesha majukumu yake kwa msingi na ufanisi.

Amesema Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake imeweza kushughulikia migogoro ya ardhi ipatayo 74 katika Mikoa ya Arusha, Chukwani, Dar es Salaam, Dodoma, Kagera, Mara, Lindi, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora ma maeneo ya Kisakasaka Zanzibar.

" Zoezi hili linaendelea kwa maeneo ya Welezo, Bavuai, Ubago, Dunga na Unguja Ukuu Zanzibar na katika maeneo haya hadi sasa jumla ya Sh Bilioni 8.01 kimetolewa na Serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi katika maeneo ya Chato, Kaboya (21KJ), Kikombo Dodoma, Mitwero Lindi, Nyabange Butiama, aidha uthamini na uhakiki umekamilika katika maeneo ya Ras Nondwa Kigoma, Nyagungulu Mwanza, Nyamisangura Tarime, Usule Tabora na Duluti Arusha. Maeneo 50 yameshafanyiwa upimaji na uthamini na ambayo uhuishaji wa mipaka na uhakiki unaendelea," Amesema Dk Stergomena.

Amesema Serikali ya awamu ya sita imewezesha Wizara ya Ulinzi kuendelea na ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa katika eneo la Kikombo jijini Dodoma ambapo ujenzi huo unatekekelezwa Kwa kutumia rasilimali fedha na wataalamu wa ndani na umefikia asilimia 70 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2022.

Kuhusu huduma za Afya, Waziri Stergomena amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Jeshi katika eneo la Msalato jijini Dodoma ambapo inashirikiana na Serikali ya Ujerumani ambapo ujenzi huo unaogharimu kiasi cha Sh Bilioni 20 inategemewa itakapokamilika iweze kutoa huduma katika ngazi ya rufaa na hivyo kuongeza uwezo wa kitabibu jijini Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia kurudishwa Jeshini kwa vijana waliokua mafunzoni zaidi ya 800 ambao walisimamishwa na Jeshi kutokana na utovu wa nidhamu Amesema Jeshi limeamua kuwarudisha vijana hao baada ya kuridhishwa na mienendo yao huko ambapo walikua.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Lawrence Tax akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma wakati akiwasilisha mafanikio ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha mwaka mmoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...