Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika lisilo la kiserikali
la Investing in Children and Strengtherning their Societies (ICS ) linalohusika
na masuala mbalimbali ikiwemo malezi na makuzi bora ya watoto,ulinzi na usalama
kwa watoto na wanawake limetoa mafunzo kwa wafanyakazi wake 22 kuwajengea uwezo
kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa
njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Programu Tumishi (Aplikesheni)
ya Parent App.
Akizungumza wakati wa mafunzo
hayo ya siku nne yaliyoanza leo Jumatatu Machi 28,2022 katika ukumbi wa
Vigimark Hotel Mjini Shinyanga, Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely
Sokoine amesema timu ya ICS inajifunza na
kujinoa kila siku kuendana na kasi ya kukua kwa teknolojia duniani.
Amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa njia ya mtandao (Tele conference) na shirika la Crown Without Borders South Africa na wafanyakazi wa ICS Tanzania wapatao 22 wanajengewa uwezo kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi mpya wa Parenting for Life Long Health (PLH).
“Mafunzo kwa wafanyakazi 22
wa Shirika la ICS kwa ajili ya kujifunza mkakati wa namna ya kutoa elimu ya
malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia
Parent App ni sehemu ya kujijengea uwezo
kabla ya kuanza utekelezaji yanafanyika kwa njia ya mtandao (Tele conference)
na shirika la Crown Without Borders South Africa. Baada ya mafunzo haya kazi ya
utekelezaji itaanza katika mkoa wa Mwanza na Shinyanga ”,amesema Kudely.
“Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kidunia wa kufikisha elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto na wanawake (The Global Parenting Initiative) . Sisi ICS tumeanza mafunzo haya ili kutekeleza mkakati huu kupitia mradi wa Parenting For Life Long Health (PLH) ambapo tunashirikiana na taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini”,ameeleza Kudely.
Amefafanua kuwa Shirika la
ICS litakuwa linafanya utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na taasisi ya
Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo
Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini na kufanya utafiti wa kina ili kutambua ni
kwa kiasi gani kufikisha elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto kwa njia ya
kidigitali na inaleta tija ili kupunguza ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
“Tunaanza utekelezaji wa mradi huu mkoani Shinyanga na Mwanza na awamu
ya kwanza tumepanga kufikia wazazi/walezi 1100 na awamu ya pili tunatarajia
kutanua utekekezaji na kufikia mikoa Zaidi ya 6 Tanzania na kufikia wazazi
/walezi wasiopungua 6000”,amesema Kudely.
Ameongeza kuwa Utekelezaji wa mpango huu umekuja kama sehemu ya ubunifu (Innovation) wa namna ya kufikisha elimu katika jamii kwa njia ya teknolojia na kuwafikia wanufaika wengi zaidi ili kuleta mabadiliko na kuchangia kuondoa ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
“Na sisi kama ICS kila
wakati tunapotekeleza afua zetu tunajifunza na kuja na ubunifu ambao unaweza
kuleta tija Zaidi katika jamii lakini pia kufanya tafiti zitakozopima na
kuthibitisha afua tunazotekeleza zinaleta matokeo chanya (Evidence Based
Intervention)”,amesema
“Sisi kama ICS na washirika wetu (Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini) tunajitahidi kila siku kuwa wabunifu na kuja na mikakati ambayo inaweza kutumia rasilimali kidogo na kuleta matokeo makubwa katika afua zetu zote tunazozitekeleza”,ameeleza.
Amefafanua kuwa Utekelezaji wa mradi huu (Pareting for Life Long Health-PLH) wa kutoa elimu ya malezi na makuzi ya bora ya mtoto kwa njia ya kijitali utachangia mpango wa dunia (The Global Parenting Initiative-GPI) wa kufikisha elimu ya malezi wa wazazi/malezi na pia mpango wa Taifa (NPA-VAWC) wa kupunguza Ukatili dhidi ya watoto wa wanawake na watoto.
“Wazazi/Walezi wengi wana simu kwa hiyo tumebuni namna ya kuwafikishia elimu kwa njia rahisi kabisa na inayotumia muda mfupi maana ParentApp mzazi/mlezi anaweza kuitumia hata wakati hayupo kwenyeInternet akajifunza na kupata ujumbe murua kabisa kuhusu malezi na makuzi bora ya watoto”,amesema Kudely.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...