Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza wakati wa kuendesha katika mfumo wa kimtandao katika kuendesha shughuli zake ili kuendana na teknolojia ya sasa.
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ameshauri Mabunge ya Afrika kujiunga na kujiendesha katika mfumo wa kimtandao katika kuendesha shughuli zake ili kuendana na teknolojia ya sasa.
Spika Tulia ameyasema hayo leo Machi 28, 2022 wakati akifungua semina ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Ramada, Jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine, amesisitiza kuwa kwa kutumia mfumo wa Bunge mtandao itawawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali za Bunge kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kujua yale yote yanayoazimiwa na Bunge lao lakini na wao pia kuwasilisha maoni na ushauri wao.
“Semina hii tunahitaji kuwajengea uwezo Wabunge kutoka Mabunge yote Afrika ili waweze kwenda kushauri kwenye nchi zao, zipo faida nyingi za kuwa na Bunge mtandao kwamaana zipo nyakati Wananchi, watafiti wanahitaji taarifa fulani za Bunge lakini zinamlazimu hadi aende Dodoma wakati angeweza kwa kutumia progam hii akayapata yote kwa wakati” amesema Spika Dkt. Tulia
Vilevile Spika Dkt. Tulia amesisitiza mfumo huo utawezesha pia kutoa uwanja mpana wa Wabunge kujadili mambo mbalimbali ya kiuchumi likiwemo suala la mapinduzi ya kilimo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...