Maadhimisho haya ya kimataifa ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi, Siku ya
Wanawake duniani ni tukio la kuimarisha dhamira ya usawa wa kijinsia na kuleta mabadiliko
chanya kwa wanawake. Duniani kote, makampuni na watu binafsi huadhimisha siku hii kwa
kusherehekea mafanikio ya wanawake huku wakitoa elimu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia, na kwa
kufanya hivyo, huvunja ubaguaji na kuchangia katika juhudi zinazolenga kujenga ulimwengu
wenye usawa.
Kama jukwaa la wanachama linalojumuisha Wakurugenzi Wakuu kutoka zaidi ya kampuni 160,
sekta mbalimbali nchini Tanzania, CEOrt kwa muda mrefu imekuwa mtetezi mkubwa wa utofauti
na ushirikishwaji. Uwakilishi wa wanawake katika uanachama umeendelea kukua kwa kiasi
kikubwa ndani ya miaka mitatu iliyopita, na ongezeko la 86% kwa viongozi wa kike ndani ya
CEOrt. Vilevile, CEOrt imedhamiria na kuweka malengo dhabiti kwa mpango wake wa uongozi
bora, CEO Apprenticeship Programme, unaotazamia kuongeza ushiriki wa wanawake kutoka
25% hadi 40% ifikapo mwaka wa 2025.
CEOrt ina furaha kumkaribisha Mhe. Balozi
Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa
mzungumzaji mkuu na Mgeni Rasmi. Balozi Mulamula atamuwakilisha Mh. Rais Samia Suluhu
Hassan, ambaye CEOrt inampongeza kwa mafanikio yake katika nafasi ya ujumuishaji wa
jinsia. Kupitia Rais Samia, viongozi wa sekta binafsi wanatambua ari na ushirikiano wa uongozi
katika kuboresha mazingira ya biashara, kuwezesha Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni
kuelekea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa. Vilevile, Raisi Samia ameonyesha mtazamo
shirikishi wa uongozi, ambao unadhihirika katika ongezeko la uwakilishi wa wanawake katika
nafasi za uongozi serikalini kwa athari endelevu katika ukuaji wa uchumi wa nchi katika miaka
ijayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, Santina Majengo-Benson, amesisitiza
dhamira ya shirika kutetea hadharani usawa wa kijinsia na utofauti. "Kuwa na wanawake katika
nafasi za uongozi ni muhimu sana. Kwa mtazamo wa kibiashara, ongezeko la uwakilishi wa
wanawake katika nyadhifa za uongozi hupelekea kuimarisha utendaji kazi - baadhi ya tafiti
zimeonyesha; kuwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kike husababisha ongezeko la asilimia tano la thamani ya soko la shirika," alisema. CEOrt ina nia ya kutumia ushawishi wao wa uongozi ili
kukuza usawa wa kijinsia kwa kusaidia uwezeshaji wa wanawake, wanawake walio katika
uongozi na kuhamasisha mwonekano chanya wa wanawake wote. Ndivyo tutakavyovunja
upendeleo kwa kweli.
Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2022 ni Vunja Upendeleo, ambayo inahimiza
ulimwengu kukomesha dhana potofu za kijinsia katika jamii, mahali pa kazi, mashuleni, na
vyuoni, katika siku hii na siku zijazo. Katika kuadhimisha siku hii na dhima, wanachama na mzungumzaji mkuu, kutoa wito kwa washiriki 'kufikiri usawa na
kuongoza kwa busara'.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...