KATIKA kuadhimisha siku ya Wanawake duniani jukwaa la Taasisi ya Wakurugenzi na Wamiliki wa Makampuni binafsi nchini (CEOrt,) waliadhimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali za kiuchumi na kushirikishana masuala ya na uongozi na athari zake katika kujenga uchumi imara wa nchi.

Ujuzi na uzoefu kupitia mazungumzo hayo yalilenga kujenga dira ya nchi katika usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa wote ambapo kwa mujibu wa tafiti za kisayansi inaelezwa kuwa ongezeko la uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi kwa kiasi kikubwa imesababisha kuimarika kwa utendaji na hii ni sababu kuu kwa sekta binafsi kusherekea siku ya Wanawake duniani.

Katika maadhimisho hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na kupokea pongezi nyingi kutoka CEOrt kwa mafanikio makubwa hasa katika nafasi ya ujumuishi ya usawa wa kijinsia katika uongozi.

Akiwakilisha salamu kutoka kwa Rais Samia, Balozi Mulamula alieleza kuwa maadhimisho hayo ni ya Siku ya Wanawake duniani ni ya kipekee kwa kuwa na Rais mwanamke anayeongoza Taifa.

Aidha Balozi Mulamula alieleza, mchango wa CEOrt  unatambuliwa katika ujenzi wa Taifa na kuwahimiza wafanyabiashara na wadau hao kutokomeza vikwazo vya ukuaji uchumi pamoja na kutoa mapendekezo juu ya masuluhisho ya kuunga mkono ustawi wa uchumi.

Kuhusiana na Siku ya Wanawake Duniani, alieleza kuwa ni wakati wa kufikiri ulimwengu sawa wa kijinsia na uwakilishi sawa wa nafasi za uongozi na kusisitiza kuwa Serikali inafanya kazi na kuchukua hatua katika kuhakikisha kuna ongezeko la ushiriki na uwakilishi wa wanawake katika nafasi mbalimbali.

"Tumeonana teuzi zilizofanywa na Mh. Rais kuna ongezeko la mabadiliko makubwa katika nafasi kwa wanawake, pekee hawezi kufanikisha hili tumuunge mkono katika kufikia usawa kwa wote kwa kutendea haki nafasi tunazozipata pamoja na kupaza sauti kwa ajili ya wengine." Amesema.

Akichangia mada katika mjadala huo Mwenyekiti Sanjay Rughani alieleza kuwa, katika kuyafikia maendeleo ni kuvaa ujasiri wa kuchukua hatua na kuendeleza usawa wa kijinsia unaleta usawa wa kijinsia ni kuendelea kupata msukumo kupitia maendeleo yanayopatikana.

Amesema, uwakilishi wa wanawake katika wanachama wa jukwaa hilo umefika asilimia 86 kwa miaka mitatu iliyopita.

Katika mjadala huo Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Jokate Mwegelo alieleza umuhimu wa kurejea katika misingi ya kufundisha maadili katika familia pamoja na jamii kushiriki maono ya usawa wa kijinsia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

Pia alifafanua umuhimu wa viongozi wanawake kutoa shuhuda zao kwa wanawake vijana ili kukuza sera hiyo kwa vizazi vijavyo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...