Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wanaume wa kata ya Mlowa halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe,wanatajwa kuwazuia wake zao kujihusisha na vyama vya siasa hali inayopelekea kuwa na idadi ndogo ya wanawake katika vyama vya siasa kwenye kata hiyo.

Hayo yamebainishwa na katibu wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kata ya Mlowa Bi,Lusia Mkaja wakati akitoa taarifa ya jumuiya kwa viongozi wa kamati ya utekelezaji UWT wilaya ya Njombe walipofika katika kata hiyo.

Bi Makaja amesema kutokana na wanawake kuzuiwa kujihusisha na maswala ya siasa imesababisha kuwa na wakati mgumu kwa viongozi kuhamasisha wanawake kujiunga na jumuiya na kupelekea kuwa na idadi ndogo ya wanachama wanaofikia 180 pekee ndani ya kata hiyo.

“Idadi ya wanachama ni 180 kwa matawi yote nah ii ni kutokana na wanawake wengi kuzuiliwa na wanaume zao kuingia kwenye saisa”alisema Bi Mkaja

Aidha amebainisha kuwa licha ya kukutana na changamoto,uongozi wa jumuiya hiyo utaendelea kuongeza elimu kwa jamii na nguvu ya ushawishi juu ya siasa ili wanawake pia waweze kugombea nafasi za uongozi ndani ya Chama na Jumuiya.

Kwa upande wake katibu wa jumuiya hiyo wilaya ya Njombe Bi,Sauda Mohamed licha ya kupongea changamoto hiyo ameagiza viongozi wa kata hiyo kuongeza nguvu ya uhamasisho ili kuongeza idadi ya wanachama huku akiwataka viongozi na wanachama kuvaa sale wanapokutana kwenye vikao au shughuli zozote za Chama na Jumuiya.

“Chama kiliona ni namna gani tunaweza kujilikana wakaweka sale na sale hizi pia zinatangaza chama kwa hiyo ni vema kuvaa sale tunapoitana kwenye vikao vyetu”alisema Bi,Sauda

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake UWT wilaya ya Njombe Beatrece Malekela,ametoa fomu kwa viongozi wa kata na kuagiza kila kiongozi kuandikisha wanachama 150 ili kuongeza idadi ya wanachama.

“Kila mmoja akatuletee wanachama 150,na tutakuja kukusanya hizi fomu baada ya siku tano kwa kuwa huu ni mkakati wetu wa kuongeza idadi ya wanachama alisema Beatrece Malekela.
Uploading: 4832256 of 6353117 bytes uploaded.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...