Na Matukio Daima Blog

UONGOZI wa kijiji cha Igoda kata ya Luhunga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na kampuni ya Foxes Treck kupitia taasisi yake ya Foxes Community and Wildlife conservation (FCWC) kwa kujitolea zaidi ya Tsh milioni 100 kujenga wodi ya wazazi na Zahanati kama uungaji mkono jitihada za Serikali .

Akizungumza jana kijijini hapo mara baada ya mfadhili huyo kutembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo ,afisa mtendaji wa kijiji cha Igoda Laines Sanga alisema kuwa kampuni ya Foxes Treck ambao ni wawezekezaji wazawa katika kijiji hicho imeendelea kusaidia shughuli mbali mbali za kimaendeleo zikiwemo za ujenzi wa miradi ya elimu ,afya na miundo mbinu ya barabara ndani ya eneo lao.


Hivyo alisema wao kama kijiji wanajivunia kuwa na mwekezaji huyo ndani ya eneo lao kwani pamoja na kufanya shughuli zake za uwekezaji ila amekuwa ni nguzo ya maendeleo ya kijiji hicho na vijiji vingine.

" Tunamshukuru sana mfadhili wetu Foxes Treck kijiji chetu kilikuwa na changamoto ya uhaba wa Zahanati ila ameweza kutujengea pamoja na kujenga nyumba za watumishi kwenye kituo hiki pia wana Igoda wanajivunia sana kuwa na mdau wetu wa maendeleo anayetujali wananchi " alisema Sanga


Kwa upande wake muuguzi mkunga wa Zahanati hiyo ya Igoda Bahati Ndelwa mbali ya kushukuru kuwepo kwenye Zahanati hiyo ila alisema uwepo wa Zanahati hiyo umesaidia sana kupunguza vifo vya akina mama wanaokwenda kujifungua kwani toka afike kituoni hapo hakujatokea kifo hata kimoja kutokana na huduma nzuri inayotolewa kwenye Zanahati hiyo iliyojengwa na mfadhili Foxes Treck .

Hata hivyo alisema changamoto kubwa ni uhaba wa watumishi kwenye Zahanati hiyo ambayo kwa sasa kuna watumishi wawili pekee hivyo ikitokea mmoja anatatizo inamlazimu mtumishi mmoja kufanya kazi zote .

Hivyo aliomba serikali kusaidia kuongeza idadi ya watumishi ili kuboresha zaidi huduma katika Zanahati hiyo.

Meneja wa FCWC Zilipa Mgeni alisema kuwa kampuni hiyo ya Foxes Treck imeendelea kusaidia miradi mbali mbali katika kata zote tatu za Ihanu ,Mdabulo na Luhunga na kuona vijiji vinavyozunguka kampuni hiyo vinasaidia miradi ya kimaendeleo.


Aidha alisema wao kama wafanyakazi wa kampuni ya Foxs Treck wanaipongeza kampuni hiyo kwa kuwa na ushirikiano mzuri na jamii pamoja na serikali kwa kujitolea kuhudumia jamii pasipo mitafaruku .

Mgeni alisema Sanjari na kujitolea kusaidia miradi ya kimaendeleo pia kampuni hiyo imeendelea kusaidia watoto wenye mazingira magumu pamoja na Yatima kupata elimu jambo ambalo limesaidia jamii hiyo kuwa na mfariji mwema .

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Foxes Treck Geoff Foxes alisema kuwa kuwa kampuni yake inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake na hivyo ndio sababu ya kujitolea kujenga Zanahati hiyo na nyumba za watumishi .

Hata hivyo alisema ili huduma ya afya iweze kuboreshwa zaidi ni lazima wahudumu wawepo wa kutosha ambao watasaidia kufanya huduma kuwa bora vinginevyo majengo pasipo watumishi hayatasaidia kuwa na huduma bora za afya .

Foxes alisema kuwa huduma bora za afya ni pamoja na uwepo wa uzazi wa mpango na kuwa katika Zanahati hiyo ameweka chumba cha uzaji wa mpango na kuwa lengo na kuona jitihada za serikali za uboreshaji wa afya zinakwenda sawa .

Pia alisema lengo la kampuni yake ni kuendelea kuiunga mkono serikali iliyopo madarakani katika kuwahudumia wananchi wanaozunguka kampuni hiyo na kampuni yake itaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi pamoja na serikali katika uchangiaji wa miradi ya kimaendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...