Na Amiri Kilagalila,Njombe
WAKULIMA wa tarafa ya Igominyi halmashauri ya mji wa Njombe wameiomba serikali kupunguza gharama ya upimaji wa udongo ili waweze kufanikisha zoezi litakalowawezesha kulima mazao kulinganga na aina ya udongo unaopatikana kwenye maeneo yao.

Akibainisha kilio cha wananchi wa tarafa hiyo wakati wa mdahalo wa ufuatiliaji na kutathmini matokeo ya uwajibikaji wa jamii katika kuboresha maendeleo ya kilimo Njombe,afisa mawasiliano wa shirika la mwamvuli wa matumaini yaani Highland Hope Umbrella (HHU) linalofanya kazi katika kata tano ndani ya tarafa hiyo bwana Robert Shejamabu amesema,licha ya changamoto hiyo iliyowasilishwa na wakulima lakini kumekuwa na idadi ndogo ya upimaji wa sampuli kulinganisha na maombi ya wananchi.

“Mwaka 2021 wamepima sampuli 40 kutokana na changamoto ya upatikanaji wa kemikali za kupimia udongo lakini maombi ya upimaji udongo yamevuka zaidi ya 100”alisema Bwana Shejamabu

Aidha kwa niaba ya shirika, wananchi wa tarafa hiyo wameipongeza serikali ya halmashauri ya mji wa Njombe kwa kusogeza huduma ya upimaji udongo kwa kununua mkoba wa kupimia udongo (Soil test Kids) ambazo zipo tatu ndani ya halmashauri hiyo.

Afisa kilimo wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Henry Kidaule amesema serikali imepokea changamoto hiyo na kubainisha kuwa halamshauri hiyo inapima udongo kwa shilingi elfu 49,000 gharama amabyo ni chini ukilinganisha na awali kabla ya kusogeza huduma hiyo mjini Njombe.

“Zamani tulikuwa tunapeleka sampuli za udongo Uyole,Sua wakati mwingine tulikuwa tunapeleka pale mafinga ikaonekana gharama kwa wakati ule ilikuwa 75 elfu mpaka laki moja na halmashauri tukapata hivyo vifaa lakini pamoja na gharama za vitendanishi sisi kama halmashauri tukawawekea unaafuu wa kulipia shilingi 49 elfu ambayo ni kiwango cha chini sana”alisema Kidaule

Vile vile bwana Kidaule amesema licha ya gharama hiyo ya upimaji wa udongo iliyopangwa na halmashauri bado kuna sehemu ya fedha ambayo amekuwa akiichangia mkurugenzi kwa ajili ya huduma hiyo kwa wakulima.
C:Afisa mawasiliano wa shirika la mwamvuli wa matumaini yaani Highland Hope Umbrella (HHU) bwana Robert Shejamabu akitoa taarifa ya tathmini ya kazi ya shirika hilo katika kazi zilizofanyika kwenye kata tano za tarafa ya Igominyi.
Afisa kilimo wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Henry Kidaule akitoa ufafanuzi juu ya gharama za upimaji wa udongo zinazofanywa na halmashauri hiyo.
Baadhi ya wakulima wakulima wakiwa kwenye mdahalo ulioitishwa na shirika la mwamvuli wa matumaini yaani Highland Hope Umbrella (HHU) katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.
Baadhi ya wajumbe wa mdahalo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mdahalo wa tathmini kufanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...