Na. Damian Kunambi, Njombe

Wanawake Wilayani Ludewa mkoani Njombe wametakiwa kutumia vyema fursa za kibiashara zilizoanza kujitokeza wilayani humo baada ya kuwepo kwa makampuni mbalimbali ya uchimbaji makaa ya mawe yaliyoanza uchimbaji huo hivi karibuni na kuonekana wafanyakazi wake kuwa na uhitaji wa huduma mbalimbali ya vyakula na malazi ambavyo kwa sasa havipatikani kwa urahisi.

Akizungumza hayo katika hafla ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika wilayani humo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Sunday Deogratias amewataka wanawake hao kuamka na kuchangamkia fursa hizo badala ya kuwapa nafasi watu kutoka katika mikoa mingine.

"Nilitembelea maeneo yaliyoanza uchimbaji makaa ya mawe, nikakutana na wafanyakazi wa hiyo migodi wakaniambia wanachangamoto kubwa ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali kama mboga mboga, mayai, kuku na vinginevyo sasa wanawake mnashindwaje kutumia hizi fursa?", Amesema Mkurugenzi.

Ameongeza kuwa atashangazwa kuona fursa hizo zinachangamkiwa na watu kutoka maeneo mengine huku wao wakiwepo hapo na kuziangalia fursa hizo kwani Ludewa kwa sasa imeanza kufunguka na huko mbele kutahitajika kuwepo na maeneo ya malazi ya kutosha.

Aidha kwa upande wa mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema wanawake wa Ludewa ni wapambanaji hivyo amewataka kuendelea kupambana kwa kasi ili kuiletea maendeleo wilaya hiyo.

Ameongeza kuwa licha ya kuwepo kwa miradi hiyo mikubwa lakini pia kuna ujenzi wa barabara ya zege ambao ujenzi wake unakaribia kufikia ukingoni lakini huku mchakato wa kumalizia vipande vya barabara hiyo vilivyobaki ukiendelea ambapo ujenzi wake kutarajiwa kuanza mwezi Mei.

Amesema hii ni moja ya fursa ambazo wanawake wanaweza kunufaika nazo kwani barabara hii itakapo kamilika itaruhusu mwingiliano mkubwa wa watu ambao watapita na kulala katika wilaya hiyo.


Afisa utumishi wa wilaya ya Ludewa Gladness Mwano (Kushoto) akimkabidhi msaada wa magodoro mkuu wa gereza la wilaya hiyo Joannes Baitange walipotembelea gereza hilo.

Wanawake wilayani Ludewa mkoani Njombe wakiwa katika maandamano ya kusherehekea siku ya wanawake duniani
Wanawake wilayani Ludewa wakiserebuka wakati wakisherehekea siku ya wanawake dunia
Baadhi ya wanawake wilayani Ludewa wakiwa wakielekea katika gereza la wilaya hiyo kwaajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...