Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Mbunifu wa mitindo wa zamani Doreen Noni chini ya kampuni ya Peter's Daughter Initiative amezindua jukwaa burudani lijulikanalo kwa jina la ‘Hadithi Hadithi’ ambalo ni maalum kutoa elimi kuhusiana na afya ya akili.

Jukwaa hilo lilizinduliwa mkoani Dodoma na mkuu wa wilaya ya Kongwa, Remedius Mwema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.

Noni alisema kuwa moja ya tatizo kubwa la afya ya akili kwa vijana ni msongo wa mawazo ambao unatokana na masuala mbalimbali iliwa pamoja na kukosa ajira pamoja na kusoma na mambo mbalimbali katika jamii.

Alisema kuwa wameamua kutumia burudani ikiwa pamoja na muziki wa kizazi kipya, maigizo, tamthilia, vichekesho na burudani nyingine ili kuondoa hali hiyo na akili kupata ‘dawa’.

Mbali ya burudani mbalimbali, wanamuziki nyota wa kizazi kipya wa mkoa wa Dodoma Medson, Meddy Voice na Baby Jeshi walipamba uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya CDA.

Kwa mujibu wa Noni, burudani ndiyo njia pekee ya kumrejesha mtu katika hali ya kawaida na mataifa mengi yameamua kutumia njia hiyo ili kutinu afya ya akili ambayo vijana wengi wanakabiliana nayo.

Alisema kuwa taasisi yao kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine kama Msalaba Mwekundu (TRCS) wana lengo la kuelimisga mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Hadithi Hadithi inahusu Afya ya akili jinsi inavyo haribu wanajamii na jinsi gani jamii iweze kuepuka tatizo hilo,Taasisi yetu imeamua kuingia katika vita hiyo na ili kuiweka jamii katika hali nzuri na kuepuka tatizo hilo,” alisema Noni.


Mwenyekiti wa Peter’s Daughter Initiative Doreen Noni (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa jukwaa la hadithi Hadithi.
Waigizaji wakicheza igizo maalum kwa ajili ya kutoe elimu kuhusiana na afya ya akili kwa jamii hasa vijana


Baadhi ya washiriki katika jukwaa la hadithi hadithi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...