Na Khadija Kalili, Chalinze
OFISI ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya kudhibibiti ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini "Ukimwi' TACAIDS imekabidhi vituo vitatu vya kutolea huduma kwa watu walioathirika na ugonjwa huo huduma itakavyokuwa ikipatikana kwenye vituo vya afya vilivyo pembezoni mwa barabara kuu vyenye thamani ya zaidi ya Sh.Bil.1 ili kuhakikisha wanapata huduma kwa uhakika ikiwemo huduma za maabara, vipimo na pia watapewa elimu ya maarifa kwa madereva wawapo safarini.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vituo hivyo katika Kituo cha Afya cha Chalinze Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Takwimu wa TACAIDS Dkt.. Jerome Philipo Kamula alisema vituo hivyo vinatarajia kutoa huduma za afya maalum kwa waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi' watakaokuwa safarini wakati wakipita naeneo ya Halmashauri ya Chalinze wapate huduma zao wakiwa safarini.

Dkt. Kamula alisema vituo hivyo katika Halmashauri hiyo vipo maeneo ya Kituo cha Afya cha Chalinze, na vituo vingine viwili vipo katika maeneo ya Mdaula ambavyo vitatoa huduma za VVU na Ukimwi kuanzia bandarini Jijini Dar es Salaam hadi Tunduma Mkoani Songwe

Alisema huduma zitakazotolewa katika vituo hivyo kuwa ni pamoja na huduma za maabara kwaajili ya kupima virusi vya ukimwi na magonjwa mengine, huduma za utoaji wa dawa, huduma za utoaji nasaha wa VVU, mashine maalum ya kuchomea taka.


" Kituo cha Maarifa cha Mdaula ni kwa ajili ya madereva wa mwendo mrefu wakiwa safarini nje ya nchi ili wapate huduma ya elimu, nasaha na madawa sambamba na jamii inayozunguka vituo hivyo wapate huduma za afya" alisema Dkt. Kamula.


"Wote tunafahamu kwamba barabara zinapitisha bidhaa na huduma lakini panapopita bidhaa na huduma pia kuna uwezekano wa maambukizi ya ukimwi nayo kuwepo kwani madereva wa malori hupumzika hapo kupata huduma na huingiliana na jamii kwahiyo tunahakikisha huduma za kinga na tiba zinakuwepo ili wale wanaohitaji wanazipata karibu kabisa pembeni mwa barabara kuu" alisema.


Alifafanua kuwa "Wale wanaohitaji au wanaotumia dawa za kufubaza virusi ARV wanaweza kuzipata wakiwa safarini kuanzia bandarini kwenda mpaka Tunduma mpakani ambapo hata wale wanaoingia nchini wakitokea nchi jirani wanapata huduma"


Dkt. Kamula alisema vituo hivyo vipo 21 katika maendeleo ya Halmashauri zilizopo pembezoni mwa barabara kuu kuanzia bandarini jijini Dar es salaam hadi Tunduma mkoani Songwe ambapo katika Mkoa wa Pwani pekee vipo vituo vinne vya aina hiyo.


Akipokea Vituo hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo alishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya kuthibiti Ukimwi TACAIDS sambamba na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza kuboresha huduma za afya katika halmashauri hiyo.


"Mwambie Rais Samia wana Chalinze tunampenda sana ametujali kwa kutupa mradi huu muhimu kwa watanzania na sisi tutaujali, tutaienzi na kuutunza maana kuhuduma sisi Chalinze tutakuwa tumenufaika sana"


Diwani wa Kata mwenyeji ya Bwilingu Nassa Ahmed Karama ameahidi kutunza vituo hivyo ili viendelee kuhudumia jamii watanzania.


Debora Rashid Viti Maalumu Tarafa ya Msoga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi wa chalinze hasa wanawake wa Chalinze kwa kuwaletea huduma mbalimbali za afya.


"Kwa kutujali wananchi wa Chalinze kauli ya Chalinze tunasema hivi alipo mama na sisi tupo" alisema Debora.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Hassan Mwinyikondo akishikilia funguo mara baada ya kukabidhiwa Kituo hicho
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Hassan Mwinyikondo akishika funguo pamoja na Diwani Kata ya Bwilingu Nassa Ahmed

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...