WAFANYAKAZI Wanawake Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametoa msaada wa mahitaji muhimu kwa watoto waliopo mahabusu ya Watoto Upanga, jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2022.
Msaada huo ni kwa ajili ya kuwafariji watoto kwa kutambua Mama zao tupo na tunawapenda kwa waliko wanapewa elimu ya kuweza kuishi vizuri na jamii.
Wanawake Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaa walikwenda Mahabusu hiyo katika Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila Mwaka Machi 8 ambapo wametoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na kuwapa faraja.
Akizungumza wakati walipotembelea kituo hicho, Mkuu wa idara ya Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge amesema watoto waliopo katika Mahabusu ya Upanga wanatakiwa kupendwa na kujaliwa kama watoto wengine.
Chuo Kikuu Mzumbe kuwasaidia watoto waliopo katika Mahabusu ya Watoto Upanga kutimiza ndoto na kutoa elimu ya biashara.
Akizungumza wakati walipotembelea Mahabusu hiyo RAS wa ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi, amesema kuwa watoto walio wengi wamesema malengo yao ni kuwa wafanyabiashara mbalimbali hivyo kama chuo watapanga ratiba kwaajili ya kuwapa elimu ya biashara watoto walio katika Mahabusu hiyo.
"Kwahiyo Baba Lao tunaomba uweke muda kwaajili ya watoto hao kujifunza ujasiliamali na namna ya kujitegemea kufanya biashara." Amesema Prof. Ngowi
Kwa upande wake Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo amesema kuwa watoto waliopo katika mahabusu hiyo wanaweza kila kitu wanachofundishwa na walezi wao, hivyo wanabadilika kila siku kutokana na ushauri wanaupata.
Amesema watoto waliopo katika Mahabusu hiyo wanafundishwa mambo mbalimbali ikiwemo msaada wa kisaikolojia pamoja na kupewa Upendo, Kutambuliwa, kupewa usalama, Kukubalika, Kusifiwa pale wanapofanya vizuri, Kuheshimiwa, Kushirikishwa, Kuaminiwa, Kulindwa na kupewa fursa ya Kucheza.
Hata hivyo amewaasa wazazi kuwapa watoto vitu mhimu na sio vitu wanavyovitaka.
Mkuu wa idara ya Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge akimkabidhi Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo baadhi yavitu vilivyotolewa na wanawake wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam leo Machi 11, 2022.
Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Proesa Hosnest Ngowi akimkabidhi, Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo vitu mbalimbali vilivyotolewa kwaajili ya kusheherekea siku ya wanawake Duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8.
Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam walipotembelea Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2022.
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam walipotembelea Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2022.
Rasi wa ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi akizungumza na watoto waliopo Mahabusu(Hawapo pichani) walipotembelea katika Mahabusu hiyo walipotembelea Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2022.
Mkuu wa idara ya Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge akizungumza na watoto waliopo Mahabusu(Hawapo pichani) walipotembelea katika Mahabusu hiyo walipotembelea Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...