Na Farida Said, Michuzi TV- Morogoro
WAZIRI wa Nishati Januari Makamba amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imetumia takribani Sh.trilioni 3.4 katika kuuendeleza mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere Hydro Power Project na mradi huo utakapokamilika utatoa fursa kwa Watanzania kupata umeme kwa bei nafuu.
Makamba amesema katika katika kipindi cha mwaka moja tangu Rais Samia Suruhu Hassani kuingia madarakani ameidhinisha na kulipa kiasi cha shilingi Tririoni 1.4 ikilinganishwa na tririoni 2. zilizokuwa zimelipwa awali huku mradi umefikia asilimia 56 kutoka asilimia 40 ya awali.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea mradi huo, Waziri Makamba amesema Wabunge wa kamati hiyo wameridhishwa na kufurahia hatua iliofikia, wamepongeza serikali , Wizara na TANESCO na Rais kwa uwezeshaji wake na idhini yake ya kutoa malipo kwa wakati.
Ameongeza kasi hiyo ya mradi imetokana kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi na uendeshaji katika mradi huo ili kuhakikisha ubora na viwango vinafikiwa.Katika mabadiliko hayo yamehusisha mfumo mzima wa usimamizi wa mradi kwa kuongeza wataalam na utaalamu zaidi, sambamba na kumhimiza mkandarasi naye aongeze wataalamu wengi zaidi wenye uzoefu mkubwa wa miradi kama hiyo .
Hata hivyo amesem walibadilisha mfumo wa mawasiliano kati ya Wizara na TANESCO ,Mkandarasi na TANESCO pamoja na Mhandisi mshauri.’Yapo mambo ambayo tunaendelea kuyafanyia kazi ambayo yapo ndani ya uwezo wetu,lengo ni kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, ili kuongeza kiwango cha umeme nchini kwa gharama nafuu "
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini , Dustan Katandula amesema kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo kwa sasa ambapo kuna tofauti kubwa na awali walipotembelea mradi huo.‘’ Tuendelee kuiomba Serikali iendelee kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mredi huo, ili maratajio ya Watanzania kuona mradi huu unakamilika kwa wakati "
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharge Chande amesema zipo changamoto chache zilizofanya maradi huo kuchelewa ikiwemo ya ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo ilisababisha ucheleweshaji wa baadhi ya vifaa, kwa sasa wanafanya tathimini ya muda gani utakaoongezeka katika mradi huo.
Ameongeza katika asilimia 56 za mradi ulipofikia hadi sasa, ina sehemu nane na dani yake, ikiwemo njia za kupitishia maji, nyumba za wafanyakazi, tuta kuu, mashine za kuzalishia umeme, kuta za kuzuia maji yasitoke na ujenzi wa daraja katika bwawa hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...