IMEELEZWA kuwa upo uwezekano mkubwa wa mabinti na vijana waliotoka kwenye mazingira magumu ambao walikata tamaa ya maisha kuwa na mafanikio makubwa ya kiuchumi iwapo watakubali kubadilika .
Hayo yameelezwa Leo mwanafunzi wa Saikolojia kutoka chuo kikuu cha Iringa Germana Chuwa wakati wa warsha ya na Saikolojia Kwa vijana 100 wanaotoka kwenye mazingira magumu kata tatu za Luhunga, Mdabulo na Ihanu wilayani Mufindi mkoani Iringa ambao ni wanufaika wa mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM)
Chuwa alisema vijana wengi toka kwenye mazingira magumu wameshindwa kusimama wenyewe baada ya kukata tamaa ya maisha kutokana na mazingira waliyokulia .
Ila alisema kupitia mradi huyo wa YAM na elimu ambayo wamekuwa wakipatiwa vijana hao watakuwa na mwango bora wa kutimiza ndoto zao ambazo walizikatisha kutokana na mazingira magumu waliyokulia.
"Hawa vijana kutokana na mafunzo haya tunayoendelea kuwapa wameanza kuonekana ni vijana wenye shauku kubwa ya kupambana kuwa na maisha bora Kwa kumiliki uchumi wao hivyo wakitoka hapa Kwa mtaji wa elimu waliopata na wakiongezwa uwezeshwaji kiasi hawa watainuka Kwa kasi na hawataanguka tena"
Hivyo aliwataka vijana hao pindi watakapo maliza mafunzo ya siku 15 wanayopatiwa kusahau mazingira ya mwanzo na kuondoka na fikra mpya ya kwenda kupigania uchumi wao .
Mshiriki God Lumwesa ambae ni mlemavu wa viungo alisema kuwa kabla ya mafunzo hayo hakuwa na ndoto ya kuja kufanya shughuli yoyote zaidi ya kutegemea kusaidiwa Kwa Kila jambo huku akiamini yeye ni mlemavu asiyeweza kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi .
Lumwesa alisema Kwa Sasa amejipanga kurudi kuanzisha shughuli ya kiuchumi na kuisimamia ili kuja kuwa msaada Kwa familia yake .
Huku Leura Nyongole akielezea mafunzo hayo kama Kinga Kwa mabinti wenzake ambao hawakufanikiwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto ya kupata mimba za utotoni .
Kwani alisema mabinti wengi walikata tamaa ya kusonga mbele kimaisha kutokana na kupata mimba wakiwa wadogo na Sasa kutokana na mafunzo hayo wanaamini watasonga mbele .
Mradi wa YAM unatekelezwa na Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa Foxes Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland na utakelekelezwa kwenye kata za Luhunga ,Ihanu na Mdabulo ni mradi utakaonufaisha vijana na watoto wanaotoka katika familia duni zaidi ya vijana 770 atika vijiji 16.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule ( wanne kutoka kushoto waliokaa akiwa na Viongozi mbali mbali na wanufaika wa mradi wa Youth Agency Mufindi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...