Na Humphrey Shao,Michuzi Tv.

Viguvugu la umoja wa watetezi wa wanawake na wasichana nchini limesema haliridhishwi na kasi ya mabadiliko ya sheria ya ndoa badala yake wanataka mswaada wa mabadiliko ya sheria hiyo kupelekwa bungeni haraka.

Katika tamko lao, leo Machi 15, 2022 wawakilishi wa muungano wa vuguvugu la kutetea haki za wanawake na wasichana wamesema hawakubaliani na msimamo wa Serikali wa kusema kwamba mchakato wa mabadiliko ya sheria ya ndoa umerudishwa kwa wananchi.

Dk Dinah Mmbaga kutoka Taasisi ya Women Fund Trust Tanzania "Kitendo cha kurudisha mchakato huu kwa wananchi ni kwenda kinyume na msingi wa utawala bora lakini pia Bunge kama chombo kilichopewa dhamana ya kutekeleza maamuzi yaliyotolewa na mahakama linakuwa halijatimiza jukumu lake la kikatiba," 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana, Initiative Rebeca Gyumi yeye amesema ndoa za utotoni ni tatizo kubwa nchini Tanzania linalosababisha wasichana kutotimiza ndoto zao hususani za kielimu huku chanzo kikitajwa kuwa ni hali duni ya maisha, mila na desturi pamoja na ukosefu wa elimu.

"Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa wasichana wawili kati ya wasichana watano wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18, hii ni hatari sana na inapelekea idadi kubwa ya wasichana wadogo kupoteza malengo yao, haki zao za msingi na wengine kupoteza maisha," anasema.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...