Na Khadija Kalili
Uongozi wa Jumuiya ya Wanawake wenye ulemavu nchini (SHIVYAWATA) wameandaa sherehe Yao ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ikiwa hii ni siku maalumu kwa ajili ya wanawake w wenye mahitaji maalumu.
Maadhimisho hayo ya siku ya wanawake kwa upande wa wanawake wenye ulemavu yamepangwa kuadhimishwa Machi 23 katika Ukumbi wa Millennium Tower Dar es Salaam.
Akifafanua lengo la kuandaa maadhimisho ya siku hii kwa wanawake wenye ulemavu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake na Watoto (SHIVYAWATA), Nuru Awadh alisema ni kuangazia mwaka mmoja wa uongozi wa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan anayetimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani mwezi Machi mwaka jana.
"Lengo la kuanzisha siku hii muhimu kwa wanawake wenye ulemavu ni kuangazia mwaka mmoja wa uongozi wa Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuelezea juhudi alizozifanya katika kutekeleza haki za wanawake na watoto hasa wenye ulemavu Ili kukuza uchumi wa haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Jumuiya ya Wanawake wenye ulemavu tunasema sambamba na kuangazia juhudi alizozifanya katika kutekeleza haki za wanawake na watoto hasa wenye ulemavu Ili kukuza uchumi wa haki na usawa kwa maendeleo endelevu"alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mweka hazina wa Jumuiya hiyo Christina Silas alisema wanawake wenye ulemavu wanasema kuwa wanamshuku sana Mheshimiwa Rais Samia kutokana na kuanzishwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum.
"Mheshimiwa Rais Samia ametoa maelekezo kwa Wizara kuchukua hatua kutatua changamoto za watu wenye ulemavu, kuteuliwa kwa watu wenye ulemavu kwenye nafasi za maamuzi,pia tunashkuru kuona kwamba zoezi la Sensa ya Taifa kuzingatia umuhimu wa kukusanya taarifa za watu wenye ulemavu, kuendelea kutolewa asilimia kumi za Halmashauri kwa ajili ya Wanawake , vijana na wenye ulemavu na kuendelea kufanya maboresho"alisema Christina.
Christina aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na mafanikio waliyoyafikia zipo changamoto nyingi wanakabiliana nazo wanawake wenye ulemavu huku akisema kuwa Machi 16 mwaka huu Mheshimiwa Rais Samia atakapokutana na viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu katika Mkutano utakaofanyika Ikulu Dodoma Mjini basi aweze kutilia mkazo na kutoa suluhisho katika changamoto wanazokabiliana nazo ambazo ni ajira kwa wanawake wenye ulemavu bado ni tatizo.
Silas alisema kuwa wanawake wenye ulemavu wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi pindi wanapokwenda kwenye vituo na hospitali Ili kupata huduma za afya hasa vyumba vya kujifungulia watoto, vitanda vya kujifungulia kutokuwa na mazingira rafiki kwa walemavu kwani huwa ni virefu sana hivyo tunaomba kwenye hospitali zetu kuwe na vitanda maalumu kwa ajili ya kujifungua walemavu kwa ujumla tunaomba pindi mlemavu anapokwenda kujifungua aruhusiwe kuwa na wasaidizi wake hata wakalimani wa lugha tofauti na ilivyo sasa.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 Kila mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...