Na. WAF - Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wanawake kuchunguza Afya zao mara kwa mara ili kuwahi kupata matibabu endapo itabainika kuwa na ugonjwa.

Waziri Ummy amesema hayo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya ubunifu wa mitindo wa mavazi ya Katty Collection yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amebainisha kuwa katika kila wagonjwa mia moja (100) wanaoumwa saratani, wagonjwa 80 saratani imeshakua katika hali ya juu na matibabu kuwa magumu.

"Naomba nitumie jukwaa hili kuwahimiza wanawake kujenga utamaduni wa kujua Afya zetu mara kwa mara pamoja na kina baba pia." Amesema Waziri Ummy

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema bado ugonjwa wa UVIKO-19 upo na kuwataka wananchi waendelea kujitokeza kupata chanjo kwa kuwa haina madhara kama baadhi ya watu wanavyosema.

Pia amesema kuna aina ya kirusi kipya kimeibuka nchini China, Japan pamoja na Korea hivyo amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari huku akisisitiza wananchi kujitokeza kupata chanjo.

"Kwa sasa kitu ambacho kinaweza kutusaidia kujikinga na UVIKO-19 ni chanjo kwa kuwa chanjo ni salama sana, nawaomba wote ambao hamjapata mkapate chanjo ili tuweze kujikinga". Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Katty Collection za kuwainua wanawake kiuchumi ameweza kuchangia vyerehani 10.

"Wanawake tunyanyuane maana Ukimuwezesha mwanamke mmoja umewawezesha watu wengi waliokuwa nyuma yake." Amesema Waziri Ummy.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...