* Waahidi kushirikiana na Serikali katika kulitangaza Taifa Barani na Afrika na nje ya mipaka

TANZANIA kupitia Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania (PRST,) watakuwa wenyeji wa mkutano mkuu wa kitaaluma Chama cha Maafisa Uhusano Barani Afrika APRA Tanzania 2022 huku wenyeji wa mkutano wakieleza fursa mbalimbali zitokanazo na mkutano huo ikiwemo kuitangaza nchi kwa kuvutia uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii pamoja na kubadilishana na uzoefu.

Hayo yameelezwa leo na Katibu Mtendaji wa PRST Ndege Makura wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa baada ya Tanzania kukidhi vigezo itakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei mwaka huu katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere pamoja na kumbi za mikutano zilizo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini humo kwa kauli mbiu ya 'One Africa, We Bring Africa in Tanzania.'

Ndege amesema, katika mkutano huo kutakuwa na matukio matatu ikiwemo la kukutana na wanafunzi wa vyuo wanaosomea fani za Uhusiano kwa Umma na habari na kuwaeleza fursa zinazopatikana ndani na nje ya nchi, mkutano wa kawaida wa wanachama, Tanzania Night ambao ni usiku wa kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania pamoja na shughuli za utalii ambapo washiriki watatembelea vivutio vya utalii vilivyopo visiwani Zanzibar.

Amesema, Hadi sasa washiriki wapatao 300 wamethibitisha ushiriki wao katika mkutano huo wa kwanza wa kitaaluma utakaozikutanisha nchi 21 za Afrika na nchi mbili za Bulgaria na Marekani.

Kwa upande wale Makamu wa Rais PRST Mary Kafyome amesema wapo tayari kushirikiana na Serikali katika kuitangaza nchi hasa katika sekta ya utalii na uwekezaji.

‘’ Tutatumia vyema fursa hii katika kuitangaza Tanzania yetu nje ya mipaka pamoja na kubadilishana uzoefu na fursa mbalimbali za uwekezaji katika nchi wanachama na wageni kutoka nje ya nchi.’’Amesema.

Vilevile amesema mkutano huo utajikita katika mwelekeo wa kulisemea vyema bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambayo Serikali ya awamu ya sita imekuwa kinara katika kuitangaza nchi katika sekta za utalii na uwekezaji.

Mkutano huo uliobeba dhumuni la kuifanya Afrika kuwa washindani kidunia utatoa fursa kwa Tanzania ikiwa mwenyeji kupata maarifa na kuwa washindani pamoja na kupata fursa ya kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji.

Wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii, mabalozi wa Nchi za Afrika wanaowakilisha nchini zao Tanzania, wanataaluma, wanahabari na wadau wa maendeleo.


Makamu wa Rais PRST Mary Kafyome akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano mkuu wa jumuiya hiyo utakaofanyika nchini Tanzania na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuitangaza Nchi kimataifa, leo jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano mkuu wa Chama cha Maafisa Uhusiano Afrika CarenTausi Mbowe akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa watatumia fursa lukuki kupitia mkutano huo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu, maarifa na kuitangaza Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania (PRST,) Ndege Makura akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano mkuu wa Maafisa Uhusiano Afrika utakaofanyika nchini Tanzania, leo jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...